1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usitishwaji wa ujenzi wa nyumba za walowezi wa kiyahudi wamalizika

27 Septemba 2010

Maelfu ya watu huko Ukingo wa Magharibi , wameandamana kusherehekea kumalizika kwa muda uliyowekwa wa kusitisha ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi.

https://p.dw.com/p/PNK0
Mlowezi wa kiyahudi akiweka bendera za Israel wakati wakisherehekea kumalizika kwa muda wa kusitisha ujenzi wa makaazi yao huko Ukingo wa MagharibiPicha: AP

Ujenzi huo ulisitishwa kwa muda wa miezi kumi ili kutoa nafasi kwa viongozi wa Israel na wale wa mamlaka ya wapalestina kuendeleza juhudi za kufufua mazungumzo ya amani katika Mashariki ya Kati.

Israel Palästinenser Gaza Ministerpräsident Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: AP

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye hakurefusha muda wa usitishwaji huo, amemtaka Rais wa Palestina Mahamoud Abbas pamoja na hatua hiyo kutorudi nyuma katika katika mazungumzo waliyoanza ya amani.

Kwa upande wake Rais Abbas amesisitiza kuwa kuzuia kuendelea kwa ujenzi wa makaazi hayo ndiyo njia pekee ya kufanikisha mazungumzo ya amani.

Akiwahutubia viongozi wa kundi la wayahudi na wanazuoni jijini Paris Ufaransa, Rais Abbas amesema mpango wa amani utakuwa ni kupoteza muda iwapo ujenzi wa makaazi hayo utaruhusiwa.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/ZPR