1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ustawi haujapunguza umasikini Afrika

21 Aprili 2013

Nchi za Afrika zinastawi katika viwango vya uchumi vya kuonewa gele na nchi za viwannda. Lakini unomi huo umeshindwa katika miaka ya karibuni kuvipunguza viwango vya umasikini miongoni mwa watu

https://p.dw.com/p/18K5U
ABUJA, NIGERIA - DECEMBER 20: In this handout image provided by the International Monetary Fund (IMF), talks with Nigerian Central Bank Governor Sanusi Lamido Sanusi (L) during a joint press conference December 20, 2011 in Lagos, Nigeria. Lagarde is on her first trip to Africa as the Managing Director and will also visit Niger. (Photo by Stephen Jaffe/IMF via Getty Images)
Nigeria Gouverneuer der Zentralbank Sanusi Lamido Sanusi mit Christine LagardePicha: Getty Images

Wataalamu wa masuala ya uchumi wamesema hayo katika tathmini yao juu mustakabal wa kiuchumi barani Afrika.

Kulingana na takwimu za Shirika la Fedha la kimataifa IMF eneo la Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara,linatarajiwa kufikia ustawi wa asilimia 5.6 mnamo mwaka huu. Nchi 18 zinatarajiwa kufikia mpaka ustawi wa takriban asilimia 6

Eneo hilo la Afrika linatazamiwa kuendelea kustawi kwa kasi imara baina ya mwaka huu wa 2013 na mwaka wa 2014. Shirika la Fedha la Kimataifa,IMF limesema nchi zenye raslimali nyingi na zile zenye vipato vya chini kadhalika, zinatarajiwa kunufaika na utashi mkubwa wa ndani.

Vitega uchumi vyaongezeka:

Benki ya dunia imesema kuwa mitaji kutoka nje iliyoekezwa moja kwa moja barani Afrika iliongezeka kwa asilimia 5.5 mwaka uliopita, wakati ambapo katika nchi nyingine zinazoendelea uwekaji wa vitega uchumi,kutoka nje ulipungua kwa asilimia 6.6

Waziri wa Fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala
Waziri wa Fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo-IwealaPicha: NICHOLAS KAMM/AFP/Getty Images

Uwiano baina ya vitega uchumi na pato jumla la ndani ni wa kiwango cha chini kabisa miongoni mwa nchi zinazoendelea. Benki ya dunia inakilinganisha kiwango hicho na kile cha kabla ya ustawi mkubwa nchini China mnamo miaka 1960 na cha India mnamo miaka ya 1980. Benki ya dunia imesema hali hiyo inaashiria ustawi zaidi katika vitega uchumi vya kuhimiza tija. Sekta za mafuta na uchimbaji wa madini ndizo zilizopo mstari wa mbele katika kuvutia vitega uchumi vya moja kwa pamoja. Lakini vitega uchumi vimestawi pia katika sekta za huduma,kama vile maji,ujenzi na katika miradi ya nishati ya umeme .

Matabaka ya kati:

Nchi zenye matabaka ya kati yanayostawi,kama vile Ghana,Nigeria,Afrika Kusini na Kenya pia zinavutia vitega uchumi katika sekta za reja reja na shughuli za benki. Asilimia 60 ya pato jumla la ndani linatokana na ukidhi wa utashi wa watu. Kwa mujibu wa tathmini ya McKinzey & Company, Waafrika wanaoishi mijini wanatumia fedha zaidi kununua nguo na chakula kuliko watu Brazil,China na India kwa wastani. Seka za mawasiliano,benki na biashara ya reja reja zinastawi.

Umasikini bado upo:

Sekta ya ujenzi pia inastawi na vitega uchumi vya watu binafsi vinaongezeka.Lakini licha ya hayo masikini wa barani Afrika,kusini mwa jangwa la Sahara, hawanufaiki. Benki Kuu ya Dunia imesema miaka 10 ya ustawi thabiti wa uchumi umepunguza umaskini kusini mwa jangwa la Sahara, lakini siyo kwa viwango vikubwa.Benki hiyo imesema ustawi barani Afrika siyo msingi wa kupunguza umasikini kulinganisha na sehemu zingine za dunia.

Ustawi utaendelea:

Licha ya unomi wa haraka katika nchi za Afrika zenye malighafi nyingi, viwango vya umasikini vinashuka kwa kasi ndogo sana . Katika tathmini yake ya hivi karibuni juu ya Afrika,Benki ya Dunia imesema bara hilo litakuwa miongoni mwa maeneo yatakayostawi kwa haraka kutokana na bei nzuri za uzalishaji na utashi wa ndani. Lakini taasisi hiyo imesema mengi yanapasa kufanyika ili kuyafungua mawezekano yote ya bara hilo.

Mwandishi: Mtullya Abdu/afpe.

Mhariri: Bruce Amani