1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utafiti wa uchumi wa S&P waonesha wasiwasi kwa kanda ya euro

6 Desemba 2011

Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, Christine Lagarde amezikaribisha jitihada za Ujerumani na Ufaransa katika kufanikisha viwango vigumu vya fedha katika kanda ya Ulaya, lakini amesema jitihada zaidi zinahitajika.

https://p.dw.com/p/13NLT
French President Nicolas Sarkozy greets German Chancellor Angela Merkel prior to their meeting at the Elysee Palace in Paris, Monday Dec. 5, 2011. The leaders of Germany and France will try to agree on Monday on a cohesive plan to help save the euro through stricter oversight of government budgets.(Foto:Remy de la Mauviniere/AP/dapd)
Kansela Merkel na Rais SarkozyPicha: dapd

Kauli hiyo inatolewa  wakati ambapo Shirika la Ukadiriaji viwango vya uchumi la latabiri kudorora kwa uchumi kwa nchi za Ulaya.

Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Taasisi ya Ulaya mjini Washington, Lagarde amesema viongozi wa Ulaya na hasa Nicolas Sarkozy na Kansela Angela Markel wameamua jambo ambalo linapaswa kusonga mbele.

Mkuu huyo wa Shirika la Fedha Duniani IMF amesema hatua hiyo peke yake haitoshi, mambo mengi yanahitajika ili kufanya mchakato wote ukabiliwe kwa ukamilifu.

Amesema ni muhimu siyo tu, kurejesha imani katika masoko lakini pia kwa wawekezaji, wateja na makampuni yote ambayo yamepanga mikakati yao kati ya mika miwili, mitatu au hata minne.

Mkuu wa IMF, Lagarde amesema tatizo lililopo sasa katika nchi hizo za Ulaya athari zake hazitaishia katika mipaka ya nchi hizo bali zitatawanyika katika pande mbalimbali za dunia.

IMF Managing Director Christine Lagarde answers questions during a press conference in Beijing, China, Thursday, Nov. 10, 2011. The head of the International Monetary Fund said Thursday that European governments need to show political clarity about the handling of their debt crisis to reassure lenders and investors. (Foto:Alexander F. Yuan/AP/dapd)
Mkuu wa IMF Christine LagardePicha: dapd

Hapo jana Sarkozy na Merkel ikiwa kabla ya mkutano wa kilele wa mgogoro wa madeni wametoa wito wa kurekebishwa kwa mkataba wa Umoja wa Ulaya utakaojumisha nchi zote 27 wanachama za umoja huo au zile zilizopo katika kanda ya sarafu ya euro ambazo zitasisitiza sheria kali ya matumizi.

Viongozi hao wameazimia kustawisha imani katika sarafu ya euro kwa kuwepo mabadiliko kadhaa likiwemo la nchi zinazotumia sarafu hiyo kupata adhabu ya moja kwa moja pale ambapo itakumwa na nakisi katika bajeti yake kwa kasi.

Hata hivyo wachambuzi wanasema mapendekezo hayo hayaoneshi mwelekeo wa namna kufanikisha maendeleo ya kukua tena kwa uchumi katika kanda ya euro na kupungua kwa gharama za kuziwezesha kwa nchi zinazokabiliwa na mzozo katika mpango muda mrefu.

Shirika la Ukadiriaji wa viwango vya uchumi la Marekani S&P limetahadhirsha kuhusu deni la mataifa ya ulaya hali ambayo inaweza kushusha  uchumi wa nchi hizo. Shirika hilo limezipanga nchi 15 za kanda ya euro kuwa katika hatari ya athari za kiuchumi.

Tangazo hilo lilitolewa muda mfupi baada ya mkutano wa viongozi wa Ujerumani na Ufaransa.

Mchumi kutoka Kituo cha Mabadiliko cha Ulaya kilichopo mjini London nchini Uingereza, Simon Tilford anasema kama alichosikia kina usahihi kabisa basi sarafu ya euro itakuwa na hatima mbaya sana.

Mwandishi: Sudi Mnette/APEAFP
Mhariri: Mohammed Khelef