1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utamaduni wa kuapishwa kwa rais wa Marekani, Obama aangalia watangulizi wake kama kioo kwake.

Sekione Kitojo19 Januari 2009

Tarehe 30, Aprili 1789 mjini New York, rais George Washington aliapa akiwa rais wa kwanza wa Marekani na kuweka msingi wa utamaduni uliodumu kwa muda wa miaka zaidi ya mia mbili sasa.

https://p.dw.com/p/Gc8v
Rais mteule Barack Obama akikumbatiana na mkewe Michelle Obama mara baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais hapo tarehe 05.11.2008 .Picha: AP

"Mungu Nisaidie". Kwa maneno haya ya kihistoria , George Washington tarehe 30 Aprili 1789 mjini New York , aliweza kuapa akiwa rais wa kwanza wa Marekani na kuweka msingi wa utamaduni uliodumu kwa muda wa miaka zaidi ya mia mbili sasa.

Kwa wakati huu rais wa Marekani hata hivyo anaapishwa tarehe 20 mwezi wa Januari, hali ambayo ilikuwa tofauti hapo zamani kwani wajumbe wa baraza la Congress walihitaji zaidi ya mwezi mmoja kuweza kufika katika mji mkuu kutoka sehemu mbali mbali za nchi hiyo kubwa. Sherehe za kuapishwa rais , zimekuwa ni utamaduni wa kisiasa, kwa rais mpya kabla ya kuingia katika Ikulu ya Marekani, White House kuelezea mambo muhimu katika utawala wake.

Kabla ya kuanza kwa sherehe za kuapishwa kwanza kunakuwa na ufyatuaji fataki na fashfashi, na halafu rais anaapishwa, wakiwapo marais wote walioshika wadhifa huo mkubwa katika taifa hilo pamoja na wajumbe wa mabaraza ya Congress. Mkononi rais anakuwa na kitabu cha Biblia, kama alivyofanya mtangulizi wa rais mteule Obama rais George W. Bush.

Mimi George Walker Bush natamka, kwamba nitatekeleza kazi za rais wa Marekani, kwa uwezo wangu wote, kuilinda na kuitetea katiba ya Marekani, Mungu nisaidie.


Barack Obama ataapa na Biblia ambayo ilitumika na Abraham Lincoln , ambaye alitoa amri wa kuachwa huru kwa watumwa na mlinzi wa umoja wa taifa hilo la Marekani.

George Washington muasisi wa taifa la Marekani aliapa mjini New York na Philadelphia, lakini baadaye shughuli zote za kuapishwa marais zilifanyika katika mji mkuu Washington DC.

Tangu kuapishwa kwa mara ya kwanza rais Ronald Reagan, mwaka 1981 sherehe hizo zimekuwa zilifanyika katika eneo la magharibi ya Ikulu ya Marekani. Katika eneo hilo inaonekana nzuri picha ya baba wa taifa hilo George Washington.

Hotuba za uzinduzi za baba wa taifa hilo Washington na Jefferson pamoja na Lincoln zimekuwa ni somo maalum kwa kila rais mpya wa Marekani, na kila kiongozi anayeingia madarakani katika hotuba yake huweka baadhi ya maneno ya kihistoria na maelezo yaliyomo katika hotuba hizo.

Kwa kawaida hotuba ya uzinduzi inalenga zaidi katika kile rais anachotaka kukishughulikia zaidi katika wakati wake wa utawala, kama alivyosema rais Bill Clinton mwaka 1997 kuhusiana na sera zake mpya za kijamii na elimu.

Alisema kwamba katika kila nyumba ya Mmarekani katika karne hii ya 21, kila mmoja ataweza kuweka chakula mezani na hapatakuwa na mtoto atakayeachwa nyuma.


Kwa kila Mmarekani kuhudhuria katika sherehe hizo za uzinduzi ni hali tofauti kabisa ya uzoefu, na kwa wengine ina maana ya matumizi makubwa. Kwa muda wa miezi kadha sasa hoteli zimejaa katika mji huo mkuu. Inawezekana sherehe zikaendelea usiku kucha na pengine hata wiki nzima.