1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utamaduni zaidi unaleta usalama zaidi Afghanistan.

Abdu Said Mtullya18 Februari 2010

Wataalamu wa mambo ya kale wa Ujerumani wachangia katika juhudi za kuleta usalama kwa njia ya utamaduni.

https://p.dw.com/p/M5BR
Mji wa Herat, nchini Afghanistan , wenye historia ya miaka 2700.Picha: flickr.com / Herat

Ujerumani inagharimia ujenzi mpya nchini Afghanistan: inatoa fedha kwa ajili ya mafunzo ya polisi, ujenzi wa barabara, lakini pia kwa ajili ya kuendeleza utamaduni wa nchi.

Tokea mwaka 2002 wafanyakazi wa taasisi ya Ujerumani inayoshughulikia mambo ya kale wamekuwapo nchini Afghanistan katika juhudi za kudumisha kumbukumbu za utamaduni.

Mtu anapolitaja jina la Afghanistan wazo la kwanza linalomjia ni juu ya vita.Na hata ikiwa mtu anazungumzia juu ya ujenzi mpya hakuna anaefikiria juu ya urithi wa utamaduni wa nchi hiyo ikiwa pamoja na majengo yenye umuhimu katika historia ya nchi. Lakini urithi huo ni muhimu katika historia na utambulisho wa nchi.

Mtaalamu wa mambo ya kale Dr. Ute Franke kutoka Ujerumani anaongoza miradi kadhaa aliyoianzisha mwenyewe nchini Afghanistan. Kwa mfano mtaalamu huyo ameelezea juhudi anazofanya katika mji wa Herat.Sehemu mojawapo katika mji mkuu Kabul.

Herat ni mji wa tokea enzi za Mfalme Alexander Mkuu(The Great).Watalaamu wa Ujerumani wa mambo ya kale wanasema kuwa mji huo una historia ya miaka 2700. Jina la mji huo linatokana na mto muhimu-Hari wenye maana ya maji ya dhahabu.

Kwa hiyo sehemu hiyo ya kale ni muhimu katika utamaduni na ustaarabu wa kiislamu .Mji huo una majengo mengi ya kumbukumbu yasiyokuwa na kifano katika mji mkuu Kabul. Pana majengo ya kuvutia ya tokea karne nyingi .

Mtaalamu wa mambo ya kale Dr. Ute Franke amesema huo ni ushuhuda wa utamaduni mkubwa wa zamani.

Lakini watu wanauliza iwapo isingekuwa bora kwa watu wa Afghanistan kupata maji safi na kuwa na nyumba bora badala ya kufikiria juu ya tunu za kihistoria.

Mtaalamu Dr. Ute Franke amesema inawezekana kufungamanisha juhudi za kudumisha kumbukumbu za utamaduni na kuleta hali bora katika maisha ya wananchi.

Na mji wa Herat umeonyesha kwamba inawezekana kuleta hali bora ya maisha sambamba na kudumisha urithi wa utamaduni.

Katika juhudi za ujenzi mpya katika sehemu hiyo ya zamani, njia zinazotumiwa na watembea kwa miguu zinatiwa lami, mfumo wa usafi wa vyoo unajengwa upya ili kuondoa hali ya uchafu wa kutisha ya hapo awali. Matanki makubwa ya kuhifadhia maji yanatolewa na kusafishwa.Wakaazi wa Herat wanafungamanisha hayo na kuboreshwa zaidi kwa maisha yao.

Mfano mwingine wa kuonyesha jinsi matunzo ya urithi wa utamaduni yanavyoenda sambamba mambo ya manufaa katika maisha ya kila siku ya wananchi ni bustani kubwa katika sehemu ya Bagh E Babur katika mji mkuu, Kabul.Mtaalamu Dr.Ute Frank amefanya kazi katika kitongoji hicho tokea mwanzo kabisa, wakati sehemu hiyo ilipokuwa gofu tupu. Lakini sasa kitongoji hicho kimekuwa sehemu inayostawi. Kutokana na maendeleo hayo sehemu hiyo sasa imo katika orodha ya shirika laelimu, sayansi na utamaduni la Unesco. Shirika hilo linafikiria kuutunukia mji huo heshima ya kuwa miongoni mwa miji bora ya utamaduni duniani.

Kwa wakaazi wa Kabul sehemu hiyo, Herat ni ishara ya mandhari yanayostawi.

Miradi ya utamaduni pia ina nyanja nyingine muhimu. Sehemu za ukumbusho zinafanyiwa ukarabati.Pamoja na kuwa muhimu kitamaduni sehemu hizo zinaleta manufaa kwa kuingiza fedha.

Watu wengi wanapatiwa nafasi za ajira kwenye sehemu hizo.

Mwandishi/Günther Birkenstock/ZR

Imetafsiriwa na:Abdu Mtullya

Mhariri:Abdul-Rahman