1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utata kuhusu uchaguzi mkuu nchini Kenya

19 Machi 2012

Nchini Kenya, bado kungali na utata kuhusu tarehe ya uchaguzi mkuu, kutokana na muongozo wa katiba mpya na serikali ya muungano iliyoundwa kufuatia mgogoro wa kisiasa mwaka 2007.

https://p.dw.com/p/14My9
Two Maasai men have their identifications checked by electoral stuff prior to voting on the draft constitution at a polling station in Suswa, some 50 km outside of Nairobi, Kenya, 04 August 2010. The government is stepping up the security, especially in the volatile Rift Valley Province, scene of the worst fighting in 2007-08 post-election violence and home to many who plan to disapprove the new draft constitution, to ensure that the country does not repeat the bloodshed that left some 1,300 dead in 2007. A survey shows more than 65 per cent of registered voters will vote in favor of the new constitution, while 25 per cent will reject it. Some 12 million Kenyans across the nation are voting in a referendum on the proposed laws, which would curve the powers of the president and devolves more power to local governments. The official result is expected to be announced by August 05. EPA/DAI KUROKAWA +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kenia Wahlen MaasaiPicha: picture-alliance/dpa

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imetangaza kuwa uchaguzi utafanyika tarehe 4 Machi 2013, baada ya Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga kushindwa kuafikiana juu ya tarehe ya uchaguzi huo. Kwa mujibu wa Barack Muluka, mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya, tarehe iliyotangazwa na tume ya uchaguzi inaendana na maelekezo ya katiba na sheria za nchi, lakini licha ya hivyo, kunaonekana kuwepo kwa ukiukwaji wa sheria,anavyosema mchambuzi huyo ni kwamba''.

kwa kiasi kikubwa (IEBC) wameweza kukiuka sheria na kuvunja mbarika kabla wakati haujawadia. Ni lazima bunge liwe limevunjwa ndipo wanapoweza kutangaza tarehe ya uchaguzi, na ni kwa mwaka huu peke yake, kwa sababu kwa miaka mingineyo yote ile tarehe ya uchaguzi imeweza kukitwa katika katiba yenyewe ikiwa ni siku ya Jumanne ya kwanza ya mwezi wa nane kila miaka mitano baada ya uchaguzi“.

Maoni ya walio wengi yanaonesha kupendelea kufanyika kwa uchaguzi mwezi wa Disemba mwaka huu kama ilivyopendekezwa na Odinga, wakitaka kuwaondowa madarakani haraka iwezekanavyo wabunge wabadhirifu, wavivu na wasiowajibika. Wakenya walio wengi wanahisi kwamba wabunge wa Kenya ambao hulipwa pesa nyingi, lakini wana mchango mdogo katika kuindeleza nchi.

Kofi Annan (katikati) mpatanishi mkuu katika mzozo wa kisiasa Kenya
Kofi Annan (katikati) mpatanishi mkuu katika mzozo wa kisiasa KenyaPicha: AP

Kenya bado yaugua

Kuhusiana na tetesi kwamba Raila Odinga huenda akajitoa katika chama chake,ili kutoa nafasi ya kuvunjika kwa serikali ya sasa na uchaguzi wa mapema kufanyika, wataalamu wanahisi kwamba si jambo linalowezekana.

Akinukuliwa na Barack Muluka, Odinga alisema “taifa hili (Kenya) bado linaugua kutokana na yale yaliyotokea miaka minne iliyopita, na halistahili kwa vyovyote vile kwenda katika uchaguzi ambao utakuwa umejikita katika muktadha wa malumbano na mambo ya majadiliano makali makali ya aina hii.

Wakati mahakama ikisubiriwa kutoa maamuzi yake juu ya rufaa ya kupinga tarehe ya uchaguzi, kuna khofu kwamba huenda mahakama hiyo ikatoa maamuzi yake kwa kuegemea upande mmoja wa serikali. Mahakama Kuu nchini Kenya iliwashangaza wengi pale ilipoamua kwamba uchaguzi utafanyika mwezi wa March mwakani na si Agosti kama ilivyoelekezwa na katiba.

Mwandishi: Hamad Omar Hamad

Mhariri: Mohammed AbdulRahman