1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utawala wa Syria umedhibiti eneo muhimu la milima ya Golan

Admin.WagnerD7 Juni 2013

Wanajeshi watiifu kwa utawala wa Syria wameliteka eneo la milima ya Golan linazitenganisha Syria na Israel kutoka mikononi mwa waasi,na duru za ulinzi zinadokeza uwezekano wa kuendelea kudhibiti maeneo mengine zaid.

https://p.dw.com/p/18lJi
Eneo la Golan
Eneo la GolanPicha: Reuters

Vifaru vya utawala wa Syria vimeonekana kwa mbali upande  mpaka wa Quneitra sehemu ambayo yalizuka mapigano makubwa kati ya  waasi na jeshi, silaha nzito nzito zikitumika. Kwa mujibu wa shirika la habari  la AFP, jeshi la Syria limechukua udhibiti wa eneo hilo na kuna uewezekano wa kutanua udhibiti huo zaidi.

Shirika la Haaki za Binaadamu la Syria lenya makao yake makuu nchini Uingrereza,limesema kuwa sasa waasi wameondoka katika eneo hilo muhimu katika milima ya Golan.Taarifa za uchunguzi zinasema askari wa Syria leo pia wamekivamia kijiji Bweida na kupelekea wakaazi wa kijiji hicho na waasi kukimbia eneo hilo muhimu la mpaka karibu na mji wa Qusair.

Mkuu wa Shirika hilo la Haki za Binadamu la Syria, Rami Abdel Rahman, amesema jeshi la Syria limetumia makombora kushambulia pia mashariki ya mji wa Bweida, maelfu ya wakaazi wake wamekimbia na maelfu ya wengine kujeruhiwa, ambao sasa wanaomba kuhifadhiwa.

Abdel Rahman amesema hali ya kiutu katika mji huo ni mbaya zaidi, kwani hakuna chakula, madawa na vifaa vya matibabu kuwa vichache na hakuna njia yoyote ya kuhudumia utitiri wa watu hao katika kijiji hicho.

Hali za kiutu bado ni tete Bweida

   Mtandao wa madakatari na wanaharakati unaripoti kuwa kwa uchache watu 500 wamejeruhiwa kijijini hapo na tayari wengine walikimbia kulekea mashariki mwa mji huo, kabla ya kuanza mashambuzi ya utawala wa Syria eneo hilo Mei 19 mwaka huu.

mkaazi wa Syria
mkaazi wa SyriaPicha: AP

Rami Abdel Rahaman amelitaka shirika la Msalaba Mwekundu  Skushinikiza utawala wa Syria kuliruhusu shirika hilo kuwasaidia majeruhi waliopo mashariki ya mji wa Bweida kuwa katika usalama na mani.

Wakati hayo yakijiri utawala wa Syria umewataka wakaazi wa Qusair kurudi katika mji wao, ingawa ripoti zinasema hakuna chochote kwenye mji huo, kwani kwa ujumla umeharibiwa wote na kugeuka jangwa.

Shirika la Msalaba Mwekundu pamoja shirika la Mwezi Mwekundu yameripoti leo kuwa yanahitaji msaada zaidi ili kuwasaida wakimbizi wa Syria, kwani hadi sasa wamepata asilimia 20 tu ya misaada hiyo, na kuomba kuongeza zaid misaada hiyo.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari mjini Amani nchini Jordan, kiongozi wa shirika la Msalaba Mwekundu, Steve McAndrew, amesema mahitaji yanaongezeka kutokana na watu kukimbia mapigano nchini Syria kila siku.

Kwa upande wake, kiongozi wa mtandao wa al-Qaida Ayman al Zawahiri amewataka wananchi wa Syria kuungana ili kumtoa madarakani Rais Assad na kuzuia mpango wa Marekani kuifanya Syria kuwa dola tiifu ya kuilinda Israel.

Mwandishi: Hashim Gulana/AFPE/RTRE &AFP

Mhariri: Mohammed Khelef