1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki kufanya kura ya maoni ya katiba

12 Septemba 2010

Raia wa Uturuki wanapiga kura ya maoni hii leo iliyo na dhamira ya kuleta mabadiliko ya katiba nchini humo.

https://p.dw.com/p/PABp
Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: AP

Lengo la shughuli hiyo nzima ni kufanya mageuzi katika mahakama isiyofuata mitazamo ya kidini inayotofautiana na uongozi unaoegemea Uislamu wa Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan.Mageuzi hayo kadhalika yana azma ya kuyapunguza madaraka ya jeshi la nchi hiyo ambalo pia mtazamo wake hauegemei misingi ya kidini.Kulingana na kura za maoni,watu wachache wanayaunga mkono mabadiliko hayo yatakayofanyiwa ibara 26 ili kuiwezesha katiba kuzifuata taratibu za Umoja wa Ulaya.

Flash-Galerie Akademiker Rückkehr in die Türkei
Eneo yaliko majengo ya Umoja wa Ulaya mjini IstanbulPicha: picture-alliance/Uwe Gerig

Kwa mujibu wa wakosoaji,azma ya chama tawala cha AK cha Waziri Mkuu Erdogan ni kuuondoa mfumo wa nchi hiyo usiofuata misingi ya kidini.Wanasiasa wengi wa vyama vya upinzani wamewatolea wito wafuasi wao kupiga kura ya kutoyaidhinisha mabadiliko hayo nacho chama kikuu cha Wakurdi kimetowa wito wa kususiwa kwa kura hiyo.