1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki kwenye mkondo unaofaa

14 Septemba 2010

Ujerumani na Umoja wa Ulaya kwa pamoja zinaiunga mkono Uturuki baada ya matokeo ya kura ya maoni ya katiba kuridhia mabadiliko.

https://p.dw.com/p/PBOo
Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: AP

Kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle,hatua hiyo ni muhimu kwa Uturuki iiliyo katika harakati za kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya.Kiasi ya asilimia 59 ya wapiga kura waliyaunga mkono mapendekezo ya kuzifanyia mabadiliko ibara 26 za katiba.

Türkischer Premierminister Erdogan mit Ehefrau Emine
Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan na mke wake Emine Erdogan:Bado ana mvuto mkubwaPicha: AP

Mabadiliko hayo yataugeuza mfumo mzima wa sheria nchini Uturuki,kuyapunguza madaraka ya jeshi pamoja na kuzilinda haki za wafanyakazi wa umma,wanawake na makundi ya kidini yaliyo na wafuasi wachache.Kulingana na Waziri Mkuu wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan,mabadiliko hayo yataiimarisha demokrasia nchini humo.Chama chake cha AK kinachoyaunga mkono mageuzi hayo pia kimefurahishwa na matokeo ya kura ya maoni ya katiba.