1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki ya hujumu PKK Iraq

23 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CfPJ

ANKARA:

Jeshi la Uturuki lilifanya mashambulio mapya hapo jana ya anga kaskazini mwa Iraq dhidi ya vituo vya wapiganaji wa kikurdi wanaotaka kujitenga kutoka Uturuki.Duru za wakurdi nchini Iraq, zimearifu kwamba ndege za kivita za uturuki zilihujumu vijiji ambavyo kwa sehemu kubwa vilikwishahamishwa wakaazi wake na kwamba hakuna aliejeruhiwa.

Jeshi la Uturuki lasema kwamba vita dhidi ya wanamgambo wa PKK ni kuwa wanalitumia eneo la mpakani kati ya Irak na Uturuki kuendesha harakati zao. Hujuma za ndege mwishoni mwa wiki iliopita zililenga sehemu hizo.