1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yakumbwa na tetemeko kubwa la ardhi

Abdu Said Mtullya24 Oktoba 2011

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uturuki, watu wapatao 1,000 wanahofiwa kupoteza maisha yao na 1090 wamejeruhiwa baada ya tetemeko la ardhi lililofikia kipimo cha 7.2 kuupiga mji wa mashariki wa Ercis.

https://p.dw.com/p/12xTn
Maafa baada ya tetemeko nchini Uturuki.
Maafa baada ya tetemeko nchini Uturuki.Picha: dapd

Tetemeko hilo lilianzia kwenye mji wa Van uliopo karibu na mpaka wa Iran.Watu 380,000 wanaishi katika mji huo wa mashariki mwa Uturuki. Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip aliutembelea mji wa Ercis uliokumbwa vibaya sana na tetemeko hilo. Majengo yapatayo 80 yalisambaratika katika mji wa huo ikiwa pamoja na bweni. Majengo mengine kumi pia yaliporomoka katika mji wa Van.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle na Rais Obama wamesema nchi zao zipo tayari kutoa misaada. Nchi za NATO na za Umoja wa Ulaya zimetoa rambirambi na pia zimesema zipo tayari kutoa misaada

Waziri Mkuu wa Uturuki Erdogan amezishukuru nchi zilizotangaza kuwa tayari kutoa misaada,ikiwa pamoja na Israel na Armenia, lakini amesema nchi yake inaweza kukabiliana na maafa hayo yenyewe.