1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uwanja wa Camp Nou uitwe Johann Cruyff?

28 Machi 2016

Kumetokea mgawanyiko wa maoni katika klabu ya Barcelona kuhusu wazo la kuupa uwanja wao unaotarajiwa kufanyiwa marekebisho makubwa wa Camp Nou, jina la nahodha wa zamani aliyefariki dunia Johann Cruyff

https://p.dw.com/p/1IKyN
Niederlande Johan Cruyff
Picha: Getty Images/AFP/K. van Weel

Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa leo kwenye mtandao wa internet. Baadhi ya vyombo vya habari vya Catalunya vimependekeza kuwa uwanja wa Camp Nou – ambao utafanyiwa marekebisho makubwa kati ya mwaka wa 2017-2021 – unapaswa sasa kupewa jina la kumuenzi Cruyff.

Hata hivyo uchunguzi huo wa maoni uliochapishwa na gazeti la kila siku la Sport umeonyesha kuwa ni asilimia 53 pekee ya wasomaji wanaounga mkono pendekezo hilo, huku 47 wakilipinga.

Cruyff aliichezea Barca kati ya mwaka wa 1973 na 1978, na akawa kocha kati ya mwaka wa 1988 nja 1996. Amefariki dunia Machi 24 akiwa na umri wa miaka 68 baada ya kuugua saratani ya mapafu kwa muda mrefu. Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu amesema atatangaza baadaye wiki hii uamuzi wake kuhusu nanmna Cruyff atakumbukwa rasmi katika klabu hiyo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Iddi Ssessanga