1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY :Baba Mtakatifu asherehekea miaka 80 ya kuzaliwa

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9Z

Baba Mtakatifu Benedict anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa ikiwa ni siku moja mapema mjini Roma.Kiongozi huyo wa kidini ametimiza miaka 80 huku ikiwa kumbukumbu ya pili tangu kuteuliwa kuwa kiongozi wa kanisa katoliki.

Maelfu ya waumini walijumuika na makadinali,maaskofu vilevile wageni mashuhuri kutoka mataifa ya kigeni kufanya sala ya pamoja katika eneo la St Peters Square.Baba Mtakatifu Benedict alizaliwa hapa Ujerumani na kuwashukuru wazazi wake Joseph ambaye ni afisa wa polisi na mamake Bi Maria.

Kiongozi huyo wa kidini ambaye pia ni mwanateolojia maarufu aliyechapisha kitabu chake cha kwanza tangu kushika wadhifa huo alimshukuru pia aliyemtangulia Marehemu Baba Mtakatifu John Paul aliyefariki Aprili 2 mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 84.

Baba Mtakatifu Benedict ni mcheza kinanda staid na katika sherehe za siku hii anapanga kuwa na maonyesho ya muziki aina ya Classical wa Dvorak na Mozart.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki alishika wadhifa huo Aprili 19 mwaka 2005 baada ya kifo cha John Paul mzaliwa wa Poland aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi wa miaka 27.