1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY : Papa ataka kuheshimiwa utu wa watoto

25 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgC

Papa Benedikt wa 16 ameongoza Misa ya Mkesha X’masi usiku wa manane leo hii katika Kanisa la St.Peter Basilica nchini Italia kwa wito wa kusaidiwa kwa watoto wanaoteseka na kudhulumiwa wakiwemo wale wanaolazimishwa kuwa omba omba na wale wanaolazamishwa kwa askari pamoja na wale wanaonyimwa chakula na mapenzi.

Katika misa yake hiyo ilioangaliwa na mamilioni ya watu kupitia vituo 73 vya televisheni katika nchi 47 duniani Papa Benedikt amesema kutokana na kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwenye zizi Mungu anawafunza kuheshimu watoto.Kiongozi huyo wa Wakristo wa madhehebu ya Wakotoliki zaidi ya bilioni moja duniani amesema mwana huyo wa Bethlehem anayaelekeza macho yao yawe kwa watoto wote ambao wanateseka na kudhulumiwa duniani wale waliozaliwa na wale ambao bado kuzaliwa akikusudia msimamo wa Kanisa Katoliki kupinga utowaji mimba.

Papa amewataka Wakristo waombe Mungu awasaidie kutimiza wajibu wao ili kuwezesha kuheshimiwa kwa utu wa watoto.

Papa huyo mzalia wa Ujerumani Joseph Ratzinger anasherekea X’masi ya pili tokea kushika wadhifa huo.