1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN: Papa Benedikt XVI akutana na Mfalme Abdullah wa Saudia Arabia

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79S

Papa Benedikt XVI na Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia wamekuwa na mkutano wa kihistoria katika Vatican.Viongozi hao wawili walijadili hali ya Wakristo wachache nchini Saudi Arabia ambako huishi kiasi ya Wakatoliki milioni moja.Wakristo nchini Saudi Arabia huruhusiwa kuabudu nyumbani kwao tu.

Wakati wa mkutano huo wa dakika 30,viongozi hao walizungumzia pia mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati uliokwama na haja ya kuwepo ushirikiano zaidi kati ya Wakristo,Waislamu na Wayahudi.