1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Venezuela :Chavez kurefusha muda ?

2 Desemba 2008

Rais Chavez wa Venezuela huenda akabadili katiba na kugombea tena ?

https://p.dw.com/p/G7jx
Rais Hugo ChavezPicha: AP

Rais Hugo Chavez wa Venezuela, anaetawala nchi hii ya Amerika Kusini tangu 1999,ana azma ya kugombea kuchaguliwa tena rais na kuiongoza Venezela hadi 2019 au ikibidi hata hadi 2021.

Kwa muujibu wa Katiba ya Venezuela, Rais anaweza tu kuchaguliwa kwsa vipindi 2 vya miaka 6 mfululizo.Hii maana yake Chavez aache madaraka ifikapo 2013. Lakini, rais anadai ""Chavismo" Uchavis bila Chavez mwenyewe hauwezekani kuwapo.Kwahivyo, lazima aongeze muda abakie madarakani kukamlisha mapinduzi yake ya ujamaa.

Rais Hugo Chavez amerudisha hujuma kali ya kimapinduzi kwa wapinzani wake walioshinda mikoa 5 kati ya yote 23 katika uchaguzi wa mwezi uliopita na kuunda serikali.Upinzani ulishinda pia i afisi ya Meya wa jiji kuu la Caracas.

Rais Chavez alisema ,

"Ikiwa tufanikishe kuongeza muda ,tufanyeni sasa tena haraka.Hebu tuanzishe vita vya kugeuza katiba Desemba mosi na nawataka kwa sababu mimi nitachangia pia-tujipatie ushindi mkuu-ushindi wa kishindo." Alitamba jana rais Hugo Chavez,mkosoaji mkubwa wa sera za Marekani na rafiki wa chanda na pete wa mzee Fidel Castro wa Cuba.

Wakati lakini haupo upande wake -asema Luis Vicente Leon, mkurugenzi wa kituo cha uchunguzi wa maoni mjini Caracas.. Akaongeza,

"kwavile sasa Upinzani unatawala mikoa tajiri na yenye wakaazi wengi,atajaribu kuhimiza kufanyika kura ya maoni juu ya swali la kuchaguliwa tena kwa rais .Hii ni kwa kuwa ,Venezuela imepitisha mwaka uliopita katika pirika pirika za uchaguzi na hatukutambua bei ya mafuta imeanguka kutoka dala 150 na kufikia dola 40 hivi sasa kwa pipa."

Rais Chavez atalazimika kukata matumizi ili kukabiliana na msukosuko huo-alisema Leon .Akaongeza kwamba, kabla msukosuko huu kuanza kuathiri watu na matokeo ya uchaguzi wa mwezi uliopita kuleta nafuu kwa Upinzani,rais Chavez ameamua kuukomea mlango asitoke madarakani kwa kurefusha kipindi cha rais.

Hatahivyo, rais Chaves aliwaambia wanadishi habari wa kigeni wiki iliopita kwamba, binafsi hatatoa pendekezo la kuchaguliwa tena,lakini anafungua mlango wazi kwa wafuasi wake kudai hivyo.

Rais Chavez alisema kwamba, alipitisha uamuzi wake baada ya kupata ripoti kwamba, wafuasi wa upinzani wa magavana wa mikoa iloshinda uchaguzi wamewahujumu na wakpanga kuwatimua madaktari wa ki-cuba wanaotoa huduma za afya katika mitaa ya masikini.Wakipanga kuondoa huduma za kuondosha ujinga wa kusoma na kuandika,majiko ya kuwapatia supu wanakofa na njaa na maduka kadhaa yanayouza vyakula vya kimsingi vinavyofidiwa bei zake ili wasiojiweza wamudu kununua.

Rais Chaves akasema na ninamnukulu,

"Hizi ni baadhi ya ishara ya kile kitakachofuata nchini Venezuela iwapo wapingamapinduzi wakija tena madarakani.Kuona kinapita nini na hatari ya mafashisti ianongezeka, Chavez hataondoka.Chavez anabakia-Mungu akipenda akiniweka hayi,nitakuwa nanyi hadi 2019 au 2021."

Mchambuzi wa maswali ya kisiasa Eduardo Semtei ameliambia shirika la habari la IPS kuwa Chavez, atabadilisha katiba ili kumruhusu kugombea tena bila kujali matokeo ya uchaguzi uliopita wa mikoa ambamo chama chake kilinyakua 52% ya kura kwa 43% ya upinzani.