1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Venezuela yatoa picha za rais Chaves

16 Februari 2013

Serikali ya Venezuela imechapisha picha za mwanzo za rais wa taifa hilo Hugo Chaves anaekabiliwa na ugonjwa wa saratani tangu afanyiwe upasuaji mjini Havana, nchini Cuba miezi miwili iliyopita.

https://p.dw.com/p/17fHm
Venezuela's President Hugo Chavez holds a copy of the newspapers as his daughters, Rosa Virginia (R) and Maria watch while recovering from cancer surgery in Havana in this photograph released by the Ministry of Information on February 15, 2013. Venezuela's government published the first pictures of cancer-stricken Chavez since his operation in Cuba more than two months ago, showing him smiling while lying in bed reading a newspaper, flanked by his two daughters. The 58-year-old socialist leader had not been seen in public since the Dec. 11 surgery, his fourth operation in less than 18 months. The government said the photos were taken in Havana on February 14, 2013. REUTERS/Ministry of Information/Handout (VENEZUELA - Tags: POLITICS PROFILE HEALTH) ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WAS PROVIDED BY A THIRD PARTY. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS PICTURE IS DISTRIBUTED EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS
Rasi wa Venezuela Hugo ChavezPicha: Reuters

Taarifa mbalimbali zilisema rais huyo wa kisoshalisti, Hugo Chaves ana shida ya kupumua na kwamba anapumua kutumua vifaa maalumu na akiwa na shida ya kupumua. Picha hizi zilizotolewa sasa zinaonamuonesha kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 58 akitabasamu lakini sura yake ikiwa kama imevimba. Alikuwa amelala kaitika kitanda cha hosiptali huku mabinti wake wawili wakiwa pembeni na mwenyewe akisoma gazeti la serikali la Cuba Granma.

Maelezo kuhusu Chaves

Picha hizo zilitolewa na mkwe wa Chaves, Waziri wa Sayansi Jorge Arreaza, ambae amekuwa akisafiri mara kwa mara kati ya Havana na Caracas kwa lengo la kuwa karibu na kiongozi huyo wa Venezuela. Akizungumza kupitia televisheni ya taifa waziri huyo amesema Chavez kwa sasa hana ile sauti yake ya kawaida. Anakuwa na wakati mgumu katika kuzungumza lakini anaweza kuelewa mambo. Anaweza kuwasilisha umuzi wake vyema. Na kuweza kuandika vyema.

Venezuela's President Hugo Chavez smiles in between his daughters, Rosa Virginia (R) and Maria while recovering from cancer surgery in Havana in this photograph released by the Ministry of Information on February 15, 2013. Venezuela's government published the first pictures of cancer-stricken Chavez since his operation in Cuba more than two months ago, showing him smiling while lying in bed reading a newspaper, flanked by his two daughters. The 58-year-old socialist leader had not been seen in public since the Dec. 11 surgery, his fourth operation in less than 18 months. The government said the photos were taken in Havana on February 14, 2013. REUTERS/Ministry of Information/Handout (VENEZUELA - Tags: POLITICS PROFILE TPX IMAGES OF THE DAY HEALTH) ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WAS PROVIDED BY A THIRD PARTY. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS PICTURE IS DISTRIBUTED EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS
Rais wa Venezuela Hugo Chavez na mabinti wakePicha: Reuters

Chavez hakuonekana hadharani, na mpaka sasa halijasikiwa lolote kutoka kwake tangu alipofanyiwa upasuaji wa nne uliyotokana na ugonjwa wa saratani Desemba 11, mwaka jana. Hata hivyo mpaka sasa sio picha hizo wala kutolewa taarifa madhubuti inayoweza kuonesha kama kiongozi huyo anaweza kurudi nyumbani au kulazimika kujiuzulu.

Makamu wa rais wa Venezuela ambae ndie anaekaimu nafasi ya urais Nicolas Maduro, alinukuliwa na vyombo vya habari hivi karibuni akisema rais Chaves yupo katika wakati mgumu sana ingawa hakutoa maelezo yoyote.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTR
Mhariri:Sekione Kitojo