1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vettel ashinda Formula One

Aboubakary Jumaa Liongo15 Novemba 2010

Ushindi wa Sebastian Vettel katika mashindanao ya Grand Prix umewasisimua wengi, na kuona kuwa Ujerumani imepiga hodi tena kwenye mbio hizo.

https://p.dw.com/p/Q8tW
Sebastian Vettel akishangilia ushindiPicha: AP

Vyombo vya habari nchini Ujerumani vimempongeza Sebastian Vettel ambaye amekuwa mjerumanai wa pili kushinda mashindano hayo ya langalanga ya Formula One huko Abu Dhabi.

Vettel mwenye umri wa miaka 23 amefuata nyayo za mjerumani mwengine Michael Schumacher ambaye alishinda mashindano hayo ya Grand Prix mara ya mwisho kati ya saba alizoshinda mwaka 2004.

Magazeti yote ya Ujerumani yameunadi ushindi wa Vettel, yakisema baada ya Schumacher sasa Ujerumani imerejea tena katika mbio za Langalanga

Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA

Mhariri:Othman Miraji