1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Hatua ya kijeshi dhidi ya Iran ni wendawazimu

15 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrY

Mkuu wa shirika la masuala ya nuklea la Umoja wa Mataifa ameitaka Iran kusitisha kuongeza urutubishaji wa uranium ili kwamba kupunguza makali ya mzozo na mataifa makubwa duniani ambayo yameitaka serikali ya Iran iifunge kabisa mpango wake huo wa nuklea.

Mohamed El Baradei mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa amesema kukwama kwa mzozo huo kati ya Iran na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kunaelekea kwenye malumbano.

Ameongeza kusema kwamba kuchukuwa hatua ya kijeshi dhidi ya Iran kutamaanisha kuwa ni uwenda wazimu. Akizungumuza katika mkutano wa IAEA ambao umeshindwa kupiga hatua yoyote ile ya maendeleo juu ya mzozo huo wa Iran amesema Iran inaendelea kukamilisha teknolojia hiyo ya kurutubisha uranium.Lakini amesema hakuna uthibitisho kwamba imevuka vikwazo vyote vya kiufundi katika teknolojia hiyo kama vile inavyodai Iran.

Serikali za mataifa ya magharibi zinahofia kwamba Iran inataka kutengeneza silaha za nuklea lakini Iran yenyewe inadai kuwa mpango wake huo ni kwa ajili ya kusambaza nishati tu.