1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Mkutano wa hali ya hewa wamalizika

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTv

Wajumbe katika mkutano wa kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa wamefikia makubaliano kwa mapana juu ya malengo yasio ya kushurutisha kwa ajili ya kupunguza utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira.

Kufuatia mazungumzo ya wiki kadhaa wamekubaliana kutambuwa haja kwa mataifa yenye maendeleo ya viwanda kupunguza gesi hizo kwa asilimia 25 hadi 40 ifikapo mwaka 2020 kwa kulinganisha na viwango vya mwaka 1990.Mazungumzo hayo ambayo yameandaliwa na Umoja wa Mataifa yalikuwa yamekusudia kuweka msingi kwa ajili ya mkutano wa hali ya hewa utakaofanyika kwenye kisiwa cha Bali nchini Indonesia hapo mwezi wa Desemba.

Madhumuni ya mkutano wa Bali ni kufikia makubaliano mapya ya kimataifa juu ya kupunguza utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira kuchukuwa nafasi ya Itifaki ya Koyoto ambayo muda wake unamalizika hapo mwaka 2012.