1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna. Shirika la Atomic halifahamu iwapo Iran inataka bomu la kinuklia.

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCM5

Kiongozi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la nishati ya Atomic , Mohammed El Baradei, amesema kuwa shirika lake bado haliwezi kutathmini iwapo Iran inataka kuwa na silaha za kinuklia.

Katika mkutano wa bodi ya magavana wa shirika hilo la IAEA mjini Vienna , El Baradei amesema kuwa baada ya uchunguzi wa muda wa miaka minne , shirika hilo limefikia hali ya mkwamo.

Ameongeza kuwa anaimani kuwa suluhisho kuhusiana na suala la kinyuklia la Iran linaweza tu kufikiwa kupitia majadiliano.