1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Shirika la IAEA kutoa ripoti yake hii leo

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBz9

Shirika la kimataifa la kupambana na usambazaji wa silaha za kinyuklia, IAEA, linatarajiwa kutoa ripoti hii leo ikiwa Iran imesitisha urutubishaji wa madini yake ya uranium.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliiwekea viwakzo Iran mwezi Machi mwaka huu kwa kushindwa kusitisha kurutubisha uranium na likasema litatoa ripoti baada ya siku 60 ikiwa Iran imetii maagizo.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linahofu Iran huenda inajaribu kwa njia ya siri kutengeneza silaha za kinyuklia, lakini serikali ya mjini Tehran imeendelea kusisitiza kwamba ina haki ya kuendelea kurutubisha uranium.

Ripoti ya shirika la IAEA itatolewa wakati Marekani ikijiandaa kumlalamikia kiongozi wa shirika hilo, Mohamed El Baradei, kuhusu pendekezo lake la kutaka Iran ihifadhi sehemu za mpango wake wa kurutubisha uranium.