1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA:IAEA yatangaza vikwazo kwa Iran

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCL6

Shirika la nguvu za Atomiki la umoja wa mataifa, limethbitisha kuikatia misaada ya kitaalam Iran, ikihofu kuwa nchi hiyo kutengeza bomu la nyuklia.

Uamuzi huo uliyotolewa na mataifa 35 wanachama wa shirika hilo, umefuatia vikwazo vilivyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa mwezi Desemba mwaka jana, kuzuia usafirishaji wa vifaa na wataalam kwenda Iran.

Iran linakuwa taifa la tatu katika historia ya miaka 50 ya shirika hilo la nguvu za atomiki duniani, kukatiwa misaada, kutokana wasi wasi wa kuweza kugeza matumizi ya nishati ya nyukilia na kutengeneza bomu.

Nchi nyingine ni Korea Kaskazini na Iraq iliyokuwa wakati huo chini ya utawala wa Saddam Hussein.