1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna:Mazungumzo ya Kosovo yaanza

21 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPx

Waakilishi wa serikali ya Serbia na wakaazi walio wengi wa asili ya Kialbania katika jimbo la Kosovo wanakutana mjini Vienna, kuujadili mpango wa mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Martti Ahtisaari kuhusu mustakbali wa jimbo hilo la Serbia. Mapendekezo yake yanaelekea kutoa mamlaka zaidi ya kiutawala kwa jimbo hilo, lakini hayaendi umbali wa kutamka moja kwa moja juu ya uhuru. Waakilishi wa jamii ya waalbania wa Kosovo imeyapongeza mapendekezo hayo, lakini maafisa wa Serbia wamesema hawatokubali kabisa Kosovo kuwa huru. Jimbo hilo limekua katika usimamizi wa umoja wa mataifa tangu 1999, baada ya kampeni ya kijeshi ya Shirika la kujihami la Magharibi-NATO, kumaliza vita vya kikabila.