1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA:Putin aishutumu Marekani

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBz2

Rais Vladmir Putin wa Urusi kwa mara nyingine tena ameshutumu mpango wa Marekani kuweka makombora ya kujihami katika ulaya ya mashariki.

Marekani inapanga kuweka makombora hayo katika Jamuhuri ya Czech na Poland, katika kile inachosema kujilinda na mashambulizi ya Iran au Korea Kaskazini.

Rais Putin hakutoa uzito juu ya uhusiano hafifu uliyopo hivi sasa kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya.Rais huyo wa Urusi alikuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Heinz Fischer na Kansela Alfred Gusenbauer.