Vijana Mubashara

Vijana Mubashara - 77 Asilimia

Ni kipindi kipya cha DW kinachokulenga wewe kijana wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kinakuweka Mubashara katika nafasi ya kutoa mchango na mawazo kuhusu maendeleo kupitia Facebook ya DW Kiswahili. Usipitwe

Claus Stäcker - Mkuu wa Idara ya lugha za Afrika

Claus Stäcker - Mkuu wa Idara ya lugha za Afrika

Vijana mubashara -77 Asilimia - Jukwaa la waafrika waliyowengi.

Asilimia 77 ya idadi ya watu katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika  ni vijana walio chini ya miaka 35. Wanakwenda shule, wanasoma na wanatafuta ajira. Pia wanataka kufunga ndoa na kuwa na majukumu. Wanawasiliana kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, WhatsApp na Instagram na kugundua kuwa sisi ni robo tatu lakini tuna machache ya kusema. Wasiwasi wetu na khofu zetu hazisikiki. Wanasiasa wetu hawatuzingatii kwa dhati.

Vijana kwa kawaida wanaongozwa na wakubwa zao au wazee wao. Robert Mugabe, rais wa zamani wa Zimbabwe alikuwa na miaka 93, kabla ya kuachia madaraka. Kwa vijana nchini mwake hakuwa tena na mwelekeo wa  kuwapa. Vijana wa Afrika wana nguvu na mawazo chungu nzima. Kizazi kipya kilicho na nguvu mpya lakini kina mitazamo hafifu. Je, wanasiasa wanafanya juhudi za kutosha kushughulikia wasiwasi wao?

Vijana wengi wana ndoto zisizotimia za kufika Ulaya au Afrika Kusini, kupitia njia hatari na zisizo za kawaida. Katika vipindi vingi, majarida na mijadala kupitia mitandao ya kijamii, DW imezingatia wasiwasi na matumaini ya vijana. Ni wazi kwamba kuna haja kubwa ya kuzungumza, kubadilishana mawazo na kuwasilisha mashaka yao kwa wahusika. Mradi wa "77Asilimia" unapaswa kuwa njia imara ya majadiliano kupitia mitandao, redio na televisheni.

Tazama vidio 01:06

Vijana Mubashara 77 Asilimia

Vijana Mubashara - " 77Asilimia" inataka kuwapa taarifa, kuwasaidia na kuwaburudisha. Vijana wenyewe ndio wanaoamua kile kitakachokuwemo. Ama iwe ni kupata vidokezo vya kutafuta kazi ama kuanzisha biashara yako mwenyewe. Iwe ni mawazo mazuri kutoka mataifa mengine au masuali magumu kwa watunga sera.

Tutajumuisha pia katuni na vichekesho - katika mradi huu wa  77 Asilimia unaweza kutabasamu na kuwa na ndoto nzuri. Ni uwanja wa Waafrika waliyowengi.

Wengi wanaijua DW zaidi kama redio, mara nyingi wazazi wameisikia Deutsche Welle. Takriban Waafrika milioni 40 wanasikiliza vipindi vya DW kila wiki, zaidi ya milioni 4 wanaifuatilia DW kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. Kanuni za msingi hazijabadilika. Tunasikiliza pande zote na kuripoti matukio kwa uwiano na haki. Vijana Mubashara –  77 Asilimia ni jukwaa ambalo tunawasikiliza Waafrika waliowengi na kuwapa sauti.

Sikiliza kila Alhamisi katika Matangazo yetu ya Asubuhi na kila Ijumaa katika Matangazo ya Mchana.

Tazama, Fuatilia na kuwa sehemu yake.

 

Mwandishi: Claus Stäcker - Mkuu wa Idara za lugha ya Afrika

Viungo vya WWW

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Albanian Shqip

Amharic አማርኛ

Arabic العربية

Bengali বাংলা

Bosnian B/H/S

Bulgarian Български

Chinese (Simplified) 简

Chinese (Traditional) 繁

Croatian Hrvatski

Dari دری

English English

French Français

German Deutsch

Greek Ελληνικά

Hausa Hausa

Hindi हिन्दी

Indonesian Bahasa Indonesia

Kiswahili Kiswahili

Macedonian Македонски

Pashto پښتو

Persian فارسی

Polish Polski

Portuguese Português para África

Portuguese Português do Brasil

Romanian Română

Russian Русский

Serbian Српски/Srpski

Spanish Español

Turkish Türkçe

Ukrainian Українська

Urdu اردو