1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana wa Ulaya wanaopigania shirikisho waungana

3 Mei 2007

Vijana wa Ulaya kutoka nchi hadi 30 wakikusanyika nchini Itali wanabadilishana fikra na maarifa na kutetea katika warsha kuwa na katiba moja ya Ulaya.

https://p.dw.com/p/CHEt

Finali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya sasa inajulikana:Mei 23 changamoto itakua marudio ya finali ya 2005 kati ya Liverpool ya uingereza na AC Milan ya Itali.Milan iliiikongoa meno jana Manchester ilipoizaba mabao 3:0 na kufuta ushindi wao wa duru ya kwanza nyumbani wa mabao 3:2.

Leo ni zamu ya Kombe jengine la Ulaya-kombe la UEFA huku timu 3 za Spain, zikichuana na moja ya Ujerumani-Werder Bremen.Bremen lakini,ina kibarua kizito leo kufuta mabao 3 iliochapwa na Espanyol huko Spian .

Watetezi wa kombe hili la UEFA Sevilla ya Spain wao kinyume na Bremen hawana kibarua kizito:wanahitaji kufuta bao 1 waliotiwa duru ya kwanza na Osasuna na ishara zote zaonesha watatamba nyumbani leo kutwaa tiketi ya finali.

Espanyol wanataka iwe finali ya waspain wenyewe kwa wenyewe,lakini kama AC Milan ilivyowatilia jana waingereza kitumbua chao mchanga kwa kuitoa Manchester isicheze finali na Liverpool, ndivyo Werder Bremen ya Ujerumani inavyopania kufanya jioni hii nyumbani.Lakini, licha ya kuwa jogoo lao Miroslav Klose limemaliza uvumi wote jana kwamba lingejiunga na Bayern munich msimu ujao,mkuki wake wakati huu si mkali hivyo kufuta mabao 3 ya Espanyola.Kwa kila hali, inaonesha finali ya Kombe la UEFA-kombe la shirikisho la dimba la Ulaya itakua kati ya Sevilla na Espanyol.

Magazeti ya italic hii leo yameitolea saluti na kuipongeza AC Milan kwa kufuta aibu waingereza walioipaka AS Roma pale Manchester ilipoizaba mabao 7-1.Milan iliifunza jana Manchester darasa la dimba kwamba, wao sio Roma.Gazzeta dello Sport –jarida la michezo nchini Itali limeiambia Ac Milan “Heko,herko,heko” kwa kila bao kati ya 3 ya hapo jana katika kikapu cha Manchester.Mabingwa hao mara 6 wa Ulaya sasa wameweka miadi kuwalipizia kisasi Liverpool kwa kuwapokonya kombe katika changamoto ya mikwaju ya penalty katika finali ya 2005.

Corriere dello Sport nalo likaandika “Milan timu ya ajabu”,kwani hii itakua finali ya 11 kwa AC Milan katika historia yake nay a 8 tangu 1989.Baada ya kutwaa kombe la dunia, wataliana wataka kutwaa kombe la Ulaya kufuta aibu na madhambi yaliotia dosari dimba lao mwaka jana kwa kashfa ya rushua na hongo katika dimba lao.

Manchester united yaweza kufuta machozi ya kulikosa kombe la Ulaya mwishoni mwa wiki hii, mradi tu wawatimue nje majirani zao Manchester city na kuondoka na taji la premier League na mapema.Manchester tayari imefungua mwanya wa pointi 5 kutoka Chelsea.

Taarifa kutoka Niamey,zasema kocha wa taifa Banna Tchanile ametimuliwa kwa Niger kushindwa kutamba katika kinya’ganyiro cha kuania tikiti ya Kombe la mwakani la bara la afrika nchini Ghana.Tchanile,raia wa Togo kwa kweli mkataba wake ulikuwa udumu hadi Septemba mwaka huu.Niger hivi sasa inaburura mkia wa kundi 3 ikiwa na pointi 1 ilipomudu sare na Uganda.