1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Vijana wakimbia Myanmar kuepuka kujiunga na jeshi

Tatu Karema
16 Februari 2024

Zaidi ya watu 1,000 wamejitokeza kwenye ubalozi wa Thailand mjini Yangon hii leo wakati vijana wakitaka kuondoka Myanmar baada ya utawala wa kijeshi kusema kuwa utawalazimisha kujiunga na jeshi.

https://p.dw.com/p/4cT2A
Myanmar Naypyitaw | Miaka 76 ya Uhuru
Kikosi maalum cha jeshi la Myanmar kwenye gwaride la heshima la Siku ya Uhuru wa nchi hiyo, 4 Januari 2024, mjini Naypyitaw.Picha: Aung Shine Oo/AP/picture alliance

Shirika la habari la AFP liliripoti kushuhudia foleni ya kati ya watu 1,000 na 2,000 katika mitaa ya karibu na ubalozi huo ikilinganishwa na idadi ya chini ya watu 100 kabla ya tangazo hilo la siku ya Jumamosi.

Ubalozi huo umesema unatoa tikiti 400 kwa siku ili kushughulikia vyema umati huo.

Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu jinsi wale watakaochaguliwa kujiunga na jeshi watakavyohudumu.

Soma zaidi: Myanmar yafanya mgomo baridi katika kumbukumbu ya mapinduzi

Jeshi hilo limesema linaandaa mikakati ya kuwapa silaha wapiganaji wanaoliunga mkono jeshi wakati linapokabiliana na wapinzani kote nchini humo.

Siku ya Jumamosi, msemaji wa jeshi, Zaw Min Tun, alisema mfumo wa huduma za kijeshi unahitajika kwa sababu ya hali inayoendelea nchini humo.