1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vimesababisha umwagaji damu mkubwa Yemen

Martin,Prema/dpa19 Septemba 2011

Nchini Yemen, vikosi vya usalama vimesababisha umwagaji damu mkubwa katika mji mkuu Sanaa.

https://p.dw.com/p/RmSB
Revolution im Jemen: Demonstrationen gegen den Präsidenten Ali Abdullah Saleh. Der Fall des Gaddafi-Regimes inspiriert die jemenitische Revolte. Die libysche Flagge ist unter den Demonstranten zu sehen. Zugeliefert am 6.9.2011 durch Dr. Abdo Jamil Al-Mikhlafy. The fall of Gaddafi and his regime gives confidence in the triumph of Yemen rebels revolt. Photo taken in : Sanaa - Yemen - september 2011. Copyright: DW / Saeed Alsoof
Rais Ali Abdullah Saleh ashinikizwa kuondoka madarakaniPicha: DW

Watu walikusanyika kwa maelfu katika maandamano ya kumpinga rais wa muda mrefu, Ali Abdullah Saleh na serikali yake. Watu walioshuhudia mashambulio hayo wamesema, hadi watu 26 wameuawa na mamia wengine wamejeruhiwa. Waandamanaji walipojaribu kuelekea makao rasmi ya rais, vikosi vilifyatua risasi. Vile vile vilitumia maji na gesi ya kutoa machozi.

Licha ya kushinikizwa kuondoka madarakani, Rais Saleh anakataa kutia saini makubaliano ya kuwakabidhi wengine madaraka. Hivi sasa, kiongozi huyo yupo Saudi Arabia kwa ajili ya matibabu ya majeraha aliyopata katika mashambulio yaliyofanywa dhidi ya makao yake rasmi mjini Sanaa mnamo mwezi wa Juni.