1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Gbagbo vyaidhibiti tena Abidjan

9 Aprili 2011

Umoja wa Mataifa umesema kuwa vikosi vinavyomtii kiongozi wa Cote d'Ivoire anayeng'ang'ania madaraka, Laurent Gbagbo, vimeudhibiti tena mji mkuu wa nchi hiyo, Abidjan.

https://p.dw.com/p/10qMG
Wanajeshi wanaomtii Laurent Gbagbo wakiwa AbidjanPicha: AP

Mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa, Alain Le Roy ameonya kuwa vikosi vya Gbagbo bado vina vifaru na silaha nyingine nzito na kwamba wako umbali wa kilometa moja tu kutoka kwenye hoteli ambayo ndio makao makuu ya kiongozi anayetambuliwa kimataifa, Alassane Ouattara.

Gbagbo amekataa kukabidhi madaraka kwa Ouattara tangu uchaguzi wa rais wa Novemba mwaka uliopita na ameendelea kubakia katika handaki kwenye makaazi yake mjini Abidjan, ambayo yamezingirwa na vikosi vya Ouattara. Mashirika ya kutoa misaada yameonya kuongezeka kwa mzozo wa kibinaadamu nchini humo.

UN Sicherheitsrat Kongo
Mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, Alain Le RoyPicha: AP

Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya jana umeondoa vikwazo dhidi ya Cote d'Ivoire, ikiwemo kuzuia bandari mbili muhimu. Ouattara aliutaka umoja huo kuiondolea vikwazo nchi hiyo ambayo ipo katika machafuko kwa lengo la kuirejesha katika hali yake ya kawaida.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (AFP,AP,RTRE)
Mhariri: Halima Nyanza