1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya israel vyafanya shambulizi gaza

Jane Nyingi5 Julai 2007

Vikosi vya Israel vimewaua wapiganaji saba wa kipalestina sita miongoni mwao wakiwa kutoka kundi la Hamas linalosimamia ukanda wa gaza.Vikosi hivyo vilikabiliana na wapiganaji hao katika kambi ya wakimbizi ya al-Maghazi iliyo kati mwa ukanda wa gaza waliojaribu kuwavurumishia grunedi.

https://p.dw.com/p/CHBY
Vikosi vya Israel katika mojawapo ya mashambulizi yake
Vikosi vya Israel katika mojawapo ya mashambulizi yakePicha: AP

Wakati wa shambulizi hilo watu 13 walijeruhiwa vibaya wakiwemo watoto. Majeshi ya Israel yamekuwa yakifanya operesheni kama hiyo mara kwa mara katika ukanda wa gaza katika harakati za kuwasaka wapiganaji wa kipalestina ambao wamekuwa wakiwashambulia waisrael kwa maroketi.

Msemaji wa kikosi hicho anasema Wapalestina hao waliauwa baada ya kukaidi amri ya majeshi ya Israel kujisalimisha.Sita kati yao waliouwa ni kutoka kundi la hamas huku mmoja ambaye hakuwa na silaha ni kutoka kundi la islamic Jihad.

Baadaye majeshi hayo ya israel yalionekana yakiharibu kituo cha polisi cha kundi hilo la hamas. waziri wa huduma za jamii nchini Israel Isaac Herzog alisema haya

"Hali katika ukanda wa gaza ni isiyovumilika hasa kwa waisraeli kwani wanashambuliwa kila siku na wapalestina.Sidhani nchi yeyote ile ingependa kuwa katika hali hii.Sasa itatulazimu kutumia nguvu na ni muhimu jamii ya kimataifa kufahamu haya mapema"

Maelfu ya Wapalestina pia wamendamana wakitaka kufanywa kwa mazumgumzo kati ya chama cha fatah na kundi la hamas ili kujaribu kutatua uhasama ambao umeibuka,kufuatia kundi la hamas kuchukua usimamizi wa ukanda wa gaza. wapalestina hao wapatao elfu tatu walibeba bendera za palestina na mabango yenye maandishi Abbas na Haniya tunataka Wapalestina wawe kitu kimoja.

Rais wa palestina Mahmoud Abbas alimfuta kazi Ismail Haniya, kiongozi wa kundi la Hamas kama waziri mkuu wa serikali ya muungano ya Hamas na fatah tarehe 4 mwezi juni saa chache kabla ya usimamizi wa ukanda wa gaza kuwa mikononi mwa kundi la Hamas.

Rais Abbas ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Fatah ameondoa uwezekano wowote wa mazungumzo na kundi la hamas na kudai lilitaka kuipindua serikali yake .

Taarrifa nyingine ni kuwa Ayman al zawahiri ambaye ni wapili kutoka kwa Osama bin laden katika uongozi wa kundi la kigaidi la alqaeda ametoa kanda ya video inayowahimiza waislamu wote kuanzisha vita vitakatifu katika mataifa ya afghanistan, iraq, somali, palestina na milima ya kaskazini mwa afrika.

Katika ukanda wa video wa muda wa dakika tisini al-zawahiri pia amekitaka chama cha fatah kinachoongozwa na rais Mahmoud Abbas kusitisha mapigano dhidi ya kundi la hamas ambalo sasa limechukua usimamizi wa ukanda wa gaza.

Ujumbe huo ni wa nane mwezi huu kutolewa na Al-zawahiri mzaliwa wa misri.