Vikosi vya Ouattara vyayashikilia makaazi ya Gbagbo
5 Aprili 2011Matangazo
Msemaji wa waasi amesema kuwa vikosi vya Ouattara vinafanya msako kwenye majengo yaliyo jirani na makaazi hao ya raisi.
Bado haijafahamika ikiwa uvamizi huu umefanikiwa kumnasa Gbagbo, ambaye ameendelea kung'ang'ania madaraka licha ya wito wa kimataifa wa kumtaka aondoke.
Wakati huo huo, helikopta za Umoja wa Mataifa zimeishambulia kambi ya wanajeshi wa Gbagbo mjini Abdijan hapo jana. Vikosi vya Ufaransa vilishiriki pia kwenye operesheni hii yenye lengo la kuziharibu silaha nzito kwenye kambi za vikosi vya Gbagbo.
Umoja wa Ulaya umeunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa, huku Rais wa Umoja huo, Herman Van Rompuy, akisema kuwa ni lazima Gbagbo aondoke madarakani ili imani ipatikane.