1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Sudan vyaondoa mzingiro

9 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRG

KHARTOUM:

Vikosi vya Serikali ya Sudan vimekubali kukomesha kuwazingira wanajeshi 61 wa kusini mwa Sudan na hivyo kutatua ugomvi uliohatarisha kuvunja yale mapatano ya amani kati ya sehemu ya kaskazini na kusini mwa Sudan.

Vikosi vya serikali ya Sudan SAF vilikizingira kikosi cha wanajeshi wa kusini mwa sudan hapo alhamisi huko kusini mwa Kordofan na kukituhumu kuvunja masharti ya makubaliano ya amani ya mwaka 2005 .

Ama kuhusu mzozo wa Dafur,Katibu mkuu wa UM Bank i Moon amepongeza Kiongozi wa Sudan Oumar Al bashir kwa ahadi yake ya kuvileta vikundi vyote pamoja kwa mkutano ujao.Alisema:

„Anasema atafanya juhudi zote kama awezavyo kuwaeta pamoja viongozi wa vikundi vyote ili kushiriki kwenye mkutano na niatoa kwahivyo shukurani zangu nyingi kwa msaada na kwa ukarimu wake.“

Alisema Katibu mkuu wa UM.