1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Syria vyaendelea kutumia mabavu

Martin,Prema/zpr3 Septemba 2011

Hadi watu 17 wameuawa na vikosi vya serikali ya Syria hapo jana, wakati waandamanaji wakiendelea kutoa mbinyo zaidi kwa serikali ya Rais Bashar al-Assad.

https://p.dw.com/p/Rjjc
epa02855868 A TV grab taken from Al Arabiya channel on 05 August 2011 shows Syrian people protesting in the city of Homs, Syria. According to media reports on 05 August, protesters took to the streets in Damascus, the southern province of Daraa and the central city of Homs following Friday prayers. According to activists, Syrian security forces opened fire and used tear gas against anti-government protesters near the capital Damascus. There were no immediate reports on casualties. EPA/AL ARABIYA / HANDOUT BEST QUALITY AVAILABLE. EPA IS USING AN IMAGE FORM AN ALTERNATIVE SOURCE, THEREFORE EPA COULD NOT CONFIRM THE EXACT DATE AND SOURCE OF THE IMAGE. HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES
Waandamanaji katika mji wa HomsPicha: picture alliance/dpa

Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la Syria, watu 8 wameuawa, baada ya vikosi vya usalama kuingilia kati kuyavunja maandamano katika viunga kadhaa vya mji mkuu Damascus. Wengine 6 waliuawa katika mji wa Homs ulio ngome ya uasi na 3 katika mji wa Deir Ezzor, mashariki mwa nchi hiyo.

Wakati huo huo, serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekubaliana kupiga marufuku kuagiza mafuta kutoka Syria. Lengo ni kumshinikiza Assad kuacha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani wa serikali. Hatua hiyo ya marufuku imepangwa kuanza Novemba 15. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa , zaidi ya watu 2,000 wameuawa tangu maandamano ya upinzani kuanza katikati ya mwezi wa Machi katika sehemu mbali mbali nchini Syria.