1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Ufaransa vyaanza kuondoka Niger

Zainab Aziz
5 Oktoba 2023

Ufaransa imeanza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Niger leo Alhamisi, miezi miwili baada ya mapinduzi ya kijeshi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

https://p.dw.com/p/4XAJE
Niger Madama Französische Soldaten
Picha: Dominique Faget/AFP

Makao makuu ya jeshi la Ufaransa lyamethibitisha kwa shirika la Habari la Ujerumani, dpa kwamba zoezi hilo limeanza rasmi.

Taarifa ya makao makuu ya jeshi inasema wanajeshi wote watarejea Ufaransa kabla ya mwisho ya mwaka huu kumalizika kwa usalama na utaratibu uliowekwa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza kuwaondoa wanajeshi wake wapatao 1,500 wa Ufaransa wiki na nusu iliyopita.

Ufaransa ilikuwa na kituo cha kijeshi katika mji mkuu wa Niger, Niamey na vituo viwili karibu mpaka wa nchi hiyo na Mali na Burkina Faso.