1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikwazo dhidi ya Gaddafi

28 Februari 2011

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaituhumu serikali ya Libya kukiuka haki za binaadam, na limepitisha azimio la kumuwekea vikwazo Gaddafi.

https://p.dw.com/p/10QSl
Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.Picha: picture alliance/dpa

Kiongozi wa Libya, Kanali Muammer Gaddafi amepuuza vikwazo vya Umoja wa mataifa dhidi yake na amesema makundi madogo ya waasi wanaopinga utawala wake watashindwa.

Massenflucht aus Libyen
Picha: DW

Siku ya Jumamosi Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa lilipitisha kwa sauti moja hatua dhidi ya kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi na jamaa zake.Vikwazo hivyo vinaanzia marufuku ya silaha, kusafiri na kufungwa akaunti zao.Taasisi hiyo muhimu ya Umoja wa Mataifa imefungua njia pia ya kuweza kuandamwa pengine Gaddafi na jamaa zake mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague kutokana na matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali nchini Libya.

Ukiukaji wa haki za binaadamu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaituhumu serikali ya mjini Tripoli kukiuka haki za binaadam. Katika maeneo yaliyokombolewa ya Libya,upande wa upinzani unaanza kujiandaa. Waziri wa zamani wa sheria Mustafa Abdul Ashleyl ametangaza kuundwa serikali ya mpito ambayo wanachama wake watatokea katika maeneo yote ya nchi hiyo. Benghazi ndio yatakayokua makao makuu ya serikali hiyo ya mpito-hadi Tripoli utakapokombolewa anasema waziri huyo wa zamani wa serikali ya Gaddafi. Kituo cha televisheni cha Al Jazeera kimeripoti kwamba vikosi tiifu kwa Gaddafi vinaendelea kudhibiti sehemu kubwa ya Tripoli.

Libyen Proteste
Picha: AP

Idadi ya watu waliofariki kwenye vurugu za karibu wiki mbili nchini Libya ni ngumu kujulikana lakini makadirio ni kuwa kati ya watu 1000 na 2000 wamefariki. Shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi, linakadiria kuwa watu laki moja wameikimbia Libya wiki iliyopita.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Ap, reuters