1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vilabu vya Bundesliga vyajiandaa na duru ya pili

5 Januari 2016

Vilabu vya daraja la kwanza katika Bundesliga vimeanza maandalizi ya sehemu ya pili ya msimu wa 2015/16 baada ya mapumziko ya sikukuu ya Krismas na mwaka mpya

https://p.dw.com/p/1HY0s
SV Darmstadt 98 Trainer Team
Picha: Getty Images/Bongarts/A. Grimm

Michuano hiyo itatimua vumbi rasmi hapo tarehe 22 mwezi huu ambapo, Hamburg SV itawakaribisha mabingwa watetezi wa Bundesliga Bayern Munich mjini Hamburg.

Viongozi wa ligi hiyo Bayern Munich wananza rasmi mazowezi hii leo mjini Munich, na wataondoka tarehe 7 mwezi huu kuelekea huko Doha Karar kwa matayarisho rasmi. Borussia Dortmund inayoshika nafasi ya pili katika Bundesliga inaanza pia mazowezi leo Jumatatu , lakini watasafiri kwenda Dubai tarehe 7 mwezi huu kwa matayarisho yatakayowachukua hadi tarehe 16 Januari.

Hertha BSC Berlin imeanza matayarisho tayari kuanzia jana Tarehe 3 Januari , lakini itasafiri kwenda kambini nchini Uturuki kuanzia tarehe 10 hadi 17.

Schalke 04 inasafiri kwenda Florida nchini Marekani kufunga kambi kwa ajili ya sehemu ya pili ya msimu, wakifuatiwa na Bayer Lecerkusen ambayo itakuwa Orlando nchini Marekani nayo ikijitayarisha kwa sehemu ya pili ya msimu huu. Klabu mbili zitafanya matayarisho yake katika bara la Afrika ambapo VFL Wolfsburg inakwenda Lagos , Nigeria kuazia Januari 9-16 na TSG Hoffenheim itakuwa huko Afrika kusini kuanzia tarehe 7- 14.

Wachezaji wamteua Costa mchezaji bora wa Bundesliga

Wakati huo huo wachezaji wa vilabu vya daraja la kwanza nchini Ujerumani, Bundesliga wamemchagua Douglas Costa wa Bayern Munich kuwa mchezaji bora wa nusu msimu, akifuatiwa na Pierre Emerick Aubameyang wa Borussia Dortmund uwanjani. Kwa mujibu wa gazeti la Kicker wachezaji 244 walioulizwa na gazeti hilo, asilimia 30.2 wamesema Costa alikuwa mchezaji bora uwanjani katika nusu msimu mwaka uliopita.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe / rtre
Mhariri: Mohammed Khelef