1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vinicius Jr. abaguliwa tena Uhispania

23 Oktoba 2023

Wingu la matukio ya ubaguzi wa rangi limeigubika Ligi kuu ya Uhispania La Liga huku Vinicius Junior akiwa mhanga kwa mara nyengine tena.

https://p.dw.com/p/4XuNh
Barcelona Länderspiel Brasilien - Guinea Vinicus
Mchezaji wa Real Madrid Vinicius JuniorPicha: Joan Monfort/AP Photo/picture alliance

Klabu ya Sevilla ilimuondoa shabiki mmoja uwanjani timu hiyo ilipokuwa ikicheza na Real Madrid, baada ya mtu huyo kufanya ishara za kibaguzi akimlenga winga wa Madrid Vinicius Junior.

Katika taarifa, Sevilla haikutaja hasa kitendo kilichofanywa na shabiki huyo wala jina la aliyelengwa ila Vinicius ambaye ni mweusi, baadae aliweka ujumbe katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii akisema ndiye aliyekuwa mlengwa.

Sevilla ilisema shabiki huyo atachukuliwa hatua kali na apigwe marufuku na uanachama wake katika klabu hiyo kufutiliwa mbali.

Vinicius ambaye mara kwa mara amelengwa na visa vya ubaguzi wa rangi amesema ilikuwa siku nyengine ya huzuni katika kandanda la Uhispania.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil Vinicius Junior
Mchezaji wa real Madrid Vinicius JuniorPicha: Harry Langer/DeFodi Images/picture alliance/dpa

Mchezaji huyo ameisifu sevilla kwa kuchukua hatua hiyo ila akasema hatua kali zaidi zinastahili kuchukuliwa na shirikisho la kandanda la Uhispania.

Chanzo: AFPE/Reuters