1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi 50 wa Ulaya kusisitiza uungaji mkono kwa Ukraine

Zainab Aziz
5 Oktoba 2023

Viongozi wakuu wa mataifa ya Ulaya wanakutana mjini Granada, Uhispania, kudadili masuala ya usafiri, nishati na akili bandia, lakini mzozo wa Ukraine na Nagorno-Karabakh itakuwa juu kwenye ajenda.

https://p.dw.com/p/4XAKd
Granada Gipfeltreffen Europäische Politische Gemeinschaft | Selenskyj
Picha: Europa Press/abaca/picture alliance

Viongozi 50 wa Ulaya wameutumia mkutano wa kilele wa usalama wa Ulaya wa Granada kusini mwa Uhispania kusisitiza juu ya kusimama pamoja na Ukraine wakati ambapo azimio la nchi za Magharibi likionekana kudhoofika kwa kiasi fulani.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kudumisha umoja huo kwa sasa ndio changamoto kuu. Licha ya msaada wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi, mapambano ya kuiokoa Ukraine kutokana na uvamizi wa Urusi kimsingi yanakabiliwa na mkwamo.

Kwa mujibu wa taarifa upinzani imara dhidi ya rais wa Urusi Vladimir Putin umeonyesha nyufa kwa sababu ya migogoro ya kisiasa ya ndani ya Marekani na pia katika Umoja wa Ulaya.

Rais wa Marekani Joe Biden ameyatolea mwito mataifa yenye nguvu duniani kuendelea kushikamana katika kuiunga mkono Ukraine wakati ambapo mustakabali wa Marekani wa kuisaidia Ukraine ukipingwa na wahafidhina wa chama cha Republican waonataka msadda wa fedha kwa Ukraine ukatwe.