1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Chama cha CCM cha Tanzania ziarani Ujerumani

Othman, Miraji26 Septemba 2008

Makada wakuu wa CCM ya Tanzania ziarani Ujerumani

https://p.dw.com/p/FPY9
Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi, CCM, wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguziPicha: AP

Ujumbe wa watu wawili kutoka Chama tawala cha Tanzania, CCM, ukiwa na katibu mwenezi wa chama hicho, John Zephania Chiligati, ambaye pia ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makaazi, na Bibi Faida Mohammed Bakar, mbunge na naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya Vijana katika CCM, umekuweko hapa Ujerumani kwa siku sita sasa kwa mwaliko wa Wakfu wa Friedrich Ebert ambao ni wa Chama cha Social Democratic, SPD. Ujumbe huo ulipata nafasi ya kuitembelea Idara hii ya matangazo ya lugha ya Kiswahili ya Deutsche Welle, Othman Miraji alizungumza na Mbunge Faida Bakar, na alimuelezea hivi kile alichojifunza katika ziara yake...