1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa dunia watakiwa kuchukua hatua za vitendo kupambana na adui njaa.

Mohammed Abdul-Rahman4 Oktoba 2007

Hivi karibuni sura iliotokeza katika umoja wa mataifa mjini Newyork ilikua ni kujumuika kwa karibu viongozi 140 wa dunia waliowasili kulihutubia baraza kuu la umoja huo. Lakini wakati wakifanya hivyo , wanaharakati walikua wakiandamana nje ya makao makuu ya umoja huo kudai hatua madhgubuti zichukuliwe kuondoa balaa la njaa duniani.

https://p.dw.com/p/C787
Jinsi njaa inavyoathiri. Huyu ni mtoto aliyekosa liche bora nchini Niger.
Jinsi njaa inavyoathiri. Huyu ni mtoto aliyekosa liche bora nchini Niger.Picha: AP

Risala ya wanaharakati hao ilikua wazi kwamba umoja wa mataifa umo katika mapambano ambayo hauwezi kushinda na kutumiza ahadi ya kupunguza kwa nusu umasikini miongoni wa wanaokabiliwa na janga. Kwa mujibu wa Shirika la kilimo na chakula la umoja wa mataifa FAO, idadi ya watu wenye njaa duniani kote imeongezeka kutoka 800 milioni mwaka 2000 hadi 854 milioni mwaka huu, 2007. Kiasi ya watu 35,000 wanakufa kwa njaa kila siku.

Viongozi wa duniani hawapaswi tu kuliweka mezani suala la njaa, lakini waliweke midomoni mwao, katika daftari zao za ratiba na kivitendo-alitamka hayo mcheza sinema wa kike kutoka Nigeria Hilda Dokubo ambaye alilalamika mno juu ya hali za wanawake barani Afrika.

Mrembo wa zamani wa Nepal na mwanaharakati anayepigania kumalizwa njaa duniani Malvika Subha, aliliambia shirika la habari la IPS kwamba anasikitshwa na hali ilivyo. Mwanaharakati huyo alikuja kuwa maarufu nchini mwake kwa kupambana dhidi ya njaa na umasikini na sasa ni msemaji wa kampeni dhidi ya njaa iliozinduliwa na wakala wa misaada Action Aid, katika nchi karibu 30 , lengo likiwa kupigania haki ya chakula iwe haki ya msingi kwa kila binaadamu.

Wanaharakati wote hao wawili Dokubo na Subha wanakubaliana kwamba wanawake katika nchi zao hubeba 50 asili mia ya mzigo panapohusika na shughuli za kilimo. Na ndiyo maana wanapigania pia kulindwa haki za wanawake. Dokubo kwa hasira anasema, hawezi kufahamu vipi viongozi watazungumzia mambo mengine zaidi ya chakula, kwa sababu njaa inauwa watu zaidi kuliko hata vita.

Katika mwaka 2000 mataifa wanachama wa umoja wa mataifa yaliahidi kutoa kipa umbele kwa vita dhidi ya njaa na umasikini. Wakati huo huo waliweka malengo ya kumaliza hali ya kukithiri kwa majanga hayo, ifikapo 2015 chini ya mpango wa malengo ya maendeleo ya milenia. Hata hivyo miaka saba baadae, maneno bado hayajageuka kuwa vitendo.

Tangu 1948, umoja wa mataifa umetambulisha kwamba haki ya kuwa na chakula cha kutosha sio tu ni haki ya kila mtu bali ni wajibu wa pamoja. Ibara ya 25 kifungu cha kwanza ya azimio la haki za binaadamu inasema „ kila mtu ana haki ya kiwango cha maisha chenye kukidhi afya na maisha yake na familia yake ikiwa ni pamoja na chakula.Lakini bado wanaharakati wanasema baadhi ya serikali zinakiuka haki ya chakula kwa kila raia.

Shirika la Action Aid, linasema litaendelea kujiunga na wataalamu na wanaharakati katika mataifa wanachama wa umoja wa mataifa, kutaka pachukuliwe hatua zinazofaa na za kivitendo kurekebisha kushindwa kwa umoja wa mataifa katika kutimiza malengo yake ya milenia.Kampeni ya kumaliza janga la njaa dunia inalenga katika kuzishinikiza serikali zianzishe na kutekeleza sheria zitakazomaliza mara moja vifo vinavyosababishwa na njaa na kuhakikisha haki msingi za jamii zinalindwa.

Jengine ni kulinda haki za wanawake, ikiwa ni pamoja na kuweza kumiliki ardhi ,na kuwa mashirika yanayohusika katika matumizi mabaya ya maji na ardhi,yawajibishwe kisheria.