1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa gazeti la Standard wahojiwa na polisi nchini Kenya

17 Aprili 2007

Nchini Kenya wakurugenzi na wahariri wa ngazi ya juu wa gazeti la The Standard walichukuliwa na askari wa usalama kuhojiwa kwa saa sita, kufuatia makala iliochapishwa jana na gazeti hilo, kuhusiana na mahojiano na mmoja wa ndugu wawili wa asili ya Armenia wamekuwa wakigonga vichwa vya habari nchini humo.

https://p.dw.com/p/CHG8

Ndugu hao wawili maarufu kama "Kina Artur" wamekuwa wakitajwa na upinzani kuwa ni kitisho kwa usalama wa taifa baada ya kuonekana kuwa karibu na maafisa wa ngazi ya juu serikalini wakidaiwa kuwa na usemi katika baadhi ya mambo, waliamriwa kuihama Kenya mwishoni mwa mwaka jana.

Mmoja wa waliohojiwa jana ni mkurugenzi wa uhariri Kwendo Opanga ambaye alizungumza na Mohamed Abdulrahman.