1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa mataifa ya Kiarabu kuhudhuria mkutano wa amani.

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSby

Cairo. Viongozi wa jumuiya ya mataifa ya Kiarabu , Arab League , wamekubali kuhudhuria mkutano wa amani ya mashariki ya kati wiki ijayo unaodhaminiwa na Marekani mjini Annapolis. Waziri wa mambo ya kigeni wa Saudi Arabia Saud al-Faisal amewaambia waandishi wa habari kufuatia mkutano wa jumuiya hiyo mjini Cairo kuwa alikuwa anasita kujiunga na mazungumzo hayo na kwamba kutakuwa hakutakuwa na hali ya mchezo wa kuigiza utakaofanywa na maafisa wa Israel.

Mataifa hayo mawili hayana uhusiano wa kidiplomasia na hii itakuwa mara ya kwanza kwa maafisa wa Saudia kukaa katika meza moja na wenzao wa taifa la Kiyahudi. Syria bado haijathibitisha ushiriki wake. Maafisa wa Syria hata hivyo, wamesema kuwa Marekani imewahakikishia kuwa suala la milima ya Golan litakuwapo katika ajenda. Hilo limekuwa moja ya masharti ya Syria kuhudhuria katika mkutano huo. Israel iliiteka milima ya Goland kutoka Syria katika vita vya siku sita vya mwaka 1967.