1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Sudan Kusini wameshindwa kuandaa uchaguzi

17 Aprili 2024

Uchaguzi mkuu nchini Sudan Kusini umeahirishwa mara kadhaa kufuatia mivutano baina ya pande hasimu zinazoshiriki kwenye serikali ya mpito.

https://p.dw.com/p/4etJY
Salva Kiir na Riek Machar mahasimu wawili wa Sudan Kusini
Salva Kiir na Riek Machar mahasimu wawili wa Sudan KusiniPicha: AFP/M. O'HAGAN

Viongozi wa kisiasa nchini Sudan Kusini wameshindwa kufikia viwango vinavyohitajika ili kuandaa uchaguzi wa haki na wa amani unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu. Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ikinukuu tathmini iliyofanwa na Umoja wa Mataifa.

Marekani imeelezea pia wasiwasi wake kuhusu ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na uwekezaji usiofaa katika taasisi muhimu za kidemokrasia katika taifa hilo changa zaidi barani Afrika na moja ya nchi masikini zaidi duniani licha ya kuwa na rasilimali ya mafuta.

Rais Salva Kiir na makamu wa kwanza wa Rais Riek Machar, ndio wapinzani wakuu na vikosi vyao vilipambana wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 2013 hadi 2018.