1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa tabaka mbili tofauti wakutana Cyprus

21 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DSRN

NICOSIA

Viongozi wa kigiriki na kituruki wa kisiwa cha Cyprus wamekubalaina kufungua kivukio muhimu katika mji mkuu wa kisiwa hicho wa Nicosia,kama ishara yenye nia ya kufufua mazungumzo ya kukiunganisha tena kisiwa hicho.Kivuko cha barabara ya Ledra,kilichoko katika eneo la katikati la maduka,kimekuwa kama alama ya mgawanyiko wa kisiwa hicho kilichoko katika bahari ya Mediterranean,uliodumu miaka 34.

Viongozi wa pande mbili wamefanya mazungumzo ya kwanza tangu Dimitris Christofias, achaguliwe kuongoza upande wa wagiriki wa kisiwa hicho mwezi uliopita. Kauli mbiu yake wakati wa kampeini ilikuwa kupatia ufumbuzi suala la mgawanyiko wa kisiwa hicho.

Christofias na kiongozi wa waturuki wa Cyprus,Mehmet Ali Talat pia wamekubaliana kuunda kamati itakayoshughulikia kuunganishwa tena kwa kisiwa hicho, na pia kuchunguza maendeleo yake katika mkutano mwingine utakaofanyika miezi mitatu ijayo.