1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Uhispania na Ujerumani wakutana Mallorca

31 Januari 2008
https://p.dw.com/p/D05Z

Viongozi wa Uhispania na Ujerumani wanakutana leo katika kisiwa cha Mallorca.

Mkutano huo wa siku moja utajadili juhudi za Umoja wa Ulaya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na maswala ya uhamiaji na nishati.

Waziri mkuu wa Uhispania, Jose Luis Rodriguez Zapatero anapanga kuujadili pamoja na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, mpango wa Umoja wa Ulaya uliozinduliwa hivi majuzi, unaozitaka nchi wanachama ziweke viwango vya kupunguza gesi za viwandani.

Ujerumani na Uhispania zimejitolea kuvifunga vinu vyao vya nyuklia wakati nchi nyingine za Ulaya zikitafakari kujenga vinu vipya.

Hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo, ombi la Uturuki kutaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya na pendekezo la rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, kutaka kuundwe muungano wa nchi zinazopakana na bahari ya Mediterenia, linalopingwa na Ujerumani na kuungwa mkono na Uhispania, ni miongoni mwa maswala yatakayojadiliwa pia katika mkutano huo wa Mallorca.