1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Vyama Vikuu vya upinzani nchini Zimbabwe wamemuonya Rais Robert Mugabe endapo atajaribu kuiba kura.

Scholastica Mazula28 Machi 2008

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha MDC Morgan Tsvangirai anaamini kuwa udanganyifu wa kura tu ndiyo utakaomzuia kumung'oa madarakani mpinzani wake mkuu Rais Robert Mugabe.

https://p.dw.com/p/DWSZ
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, alipowasili kwenye Mkutano wa Nchi za Umoja wa Ulaya na Afika uliofanyika Lisbon.Picha: AP

Hivi karibuni Rais Mugabe alisema kamwe maishani mwake ilihali yeye yuko hai, Tsvangirani hatoshika madaraka.

Morgan Tsvangirai aliyekabiliwa mara mbili na mashitaka ya uhaini na kupigwa vibaya na vikosi vya usalama na chama chake kuwa na mgawanyo mkubwa ameweza kuonyesha kuwa anakipaji cha kujichomoza kisiasa.

Kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha MDC, amekuwa mpinzani Mkuu wa Rais Robert Mugabe tangu miaka ya 1990, amekuwa akisisitiza kwamba alikuwa mshindi wa haki katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2002 ambao alipata kura milioni moja nukta mbili chini ya Mugabe ambaye alishinda kwa kura milioni moja nukta sita.

Tsvangirai katika kampeni zake amenukuliwa akisema kwamba ni lazima chama chake kishinde pamoja na kwamba Rais Mugabe hataruhusu mtu yeyote ashinde badala yake lakini anauhakika kwamba katika uchaguzi wa kesho watashinda.

Wakati huohuo mgombea mwingine wa upinzani Simba Makoni ambaye Rais Mugabe alimshutumu kama ni kahaba wa Kisiasa, amesema atahitaji zaidi ya muongo mmoja kurekebisha uchumi wa nchi hiyo ulioteketea ikiwa atafanikiwa kumuondoa mkuu wake wa zamani.

Tangu Makoni ajihuzuru kama Waziri wa fedha mwaka 2002, uchumi wa Zimbabwe umekuwa ukidhoofika na ughali wa maisha hivi sasa umezidi asilimia laki moja, wakati huohuo zaidi ya asilimia Themanini ya raia wake hawana ajira.

Makoni mwenye umri wa miaka 58 amesema ni muhimu kukabiliana na matatizo yanayoikumba nchi hiyo ikiwa ni pamoja na mizozo ya chakula, maji na nishati.

Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 84 na anayewania nafasi nyingine ya miaka mitano ya urais amekuwa akitazawa totauti na raia wa Zimbabwe wengine wakimuona kama mkombozi na wengine kama dikiteta wa kiafrika aliyebobea.

Kesho Zimbabwe itafanya uchaguzi wake ambao rais Mugabe anatumaini kuongeza muda wake wa miaka 28 akiwa kiongozi wa nchi hiyo.

Wagombea wote watatu wenye upinzani mkubwa katika uchaguzi Mkuu nchini humo wanafanya kampeni zao za mwisho za kuomba kura za uchaguzi ambao huwenda ukamwondoa madarakani rais Robert Mugabe.

Tayari Tsvangirai amemuonya Mugabe kuwa endapo atajaribu kuiba kura katika uchaguzi wa kesho basi hali ya mambo itazidi kuwa mbaya nchini humo.