Vipaji ajabu vya pua za wanyama
Sisi binadamu hutumia pua zetu kunusia na kuvutia pumzi, na hazina nguvu sana ya kunukiliza. Baadhi ya wanyama pua zao zina nguvu sana. Hawa hapa wanyama sita wenye pua zenye nguvu kubwa ya kunukiliza .
Pua ya Chifu
Pua ya Chifu Ala! Mimi ndie mkuu hapa! Inavuma pua ya rangi nyingi ya sokwe dume anayeitwa Mandrill. Masokwe dume wanaotawala wana rangi changamfu kuliko sokwe duni. Sokwe wa aina ya Mandrill wakikasirika au wakitaka kufanya kitendo cha ngono, sehemu ya buluu ya pua yao huzidi kuwa kubwa. Wekundu katika pua unatokana na mzunguko wa damu kuwa juu.
Pua ya kazi zote
Tembo wanatumia pua yao kwa shughuli mbalimbali kama vile kupiga tarumbeta, kunukizia harufu, kishikio, kuoga au kuogelea. Kusema kweli mkonga wa tembo unatumika kama mdomo wa juu na pua wakati huo huo. Na pia unatumika kama sehemu ya mawasiliano, kwa mfano wakati anapopiga kelele. Pia mkonga wa tembo unatumika kunukizia harufa za tembo jike wakati wa kukutana.
Pua ya mtokezo wa kupandana
Pua ya mtokezo wa kupandana Tembo huyu wa baharini amepata jina lake kutokana na pua yake iliyopinda, ambayo inaweza kukumbusha mkonga wa tembo. Pua yake inaning'inia hadi chini ya mdomo wake. Wakati wa msimu wa kupandana mnyama huyu dume hupaka mdomo wake damu na kutoa sauti kali kwa ajili ya kuwafukuza madume wengine. Majike na madume wote huvuta unyenyevu kupitia pua zao .
Pua vs Mwiba
Kimoja ya chakula pendwa zaidi kwa samaki huyu aitwaye "triggerfish" ni misumbi wa baharini. Hivyo ili kuhakikisha hachomwi na miiba hiyo, samaki huyo aliota pua refu ambayo anaitumia pia kupata utamu wa ndani wa misumbi hao. Pia samaki huyu hutumia pua yake kama pomba la maji na kuwalenga misumbi ili apate kuwala.
Pua kama bomba
Kinachoonekana kama pua ndefu kupita maelezo ni bomba la mnyama huyo mla mchwa. Pua yake halisi iko kwenye ncha cha bomba hilo nahutumia pua yake kunusa na kutafuta chakula, hususani mchwa na kumbikumbi. Anapopata chembe ya ladha, myama huyo huvuta ulimi wake wa inchi 35 wenye gundi na kugandisha chakula chake kwenye ulimi huo - mara 160 kila dakika.
Pua inayofanana na plagi ya umeme
Mnyama mwenye pua kama hii si mwengine ila ni nguruwe. Wengi huiona pua ya ngurue kuwa mbaya sana, lakini ni nyeti sana. Ina hisia nyingi na inanusa kitu kutoka umbali wa sentimita 50 chini ya udongo.
Pua ya kunusa
Mbwa wenye pua inayokaa kama mraba wameonekana kwa mara ya kwanza China na mfalme wakati huo ndie aliyekuwa nae mbwa wa aina hiyo. Baadae mbwa wa aina hiyo walikuwa maarufu miongoni mwa wanawake matajiri waliochorwa katika picha. Mbwa wa aina hii wametokana na kuchanganya mbegu ya aina ya mbwa tofauti. Lakini tabia hii inawafanya mbwa hawa kuwa dhaifu na kuwa na magonjwa mengi.