1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vipi taasisi za Kikristo na Kiislamu husaidia jamii

P.Martin30 Mei 2008

Je,Ukristo na Uislamu hulingana wapi na hutofautiana wapi?Hayo ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa na wajumbe wa dini zote mbili katika mkutano unaoadhimisha Siku ya Wakatoliki ya Ujerumani mjini Osnabrück.

https://p.dw.com/p/E4rJ
Eine Fahne des 97. Deutschen Katholikentages weht am Dienstag, 20. Mai 2008, vor der Kirche St. Johann in Kloster Oesede bei Osnabruck. Unter dem Motto "Du fuehrst uns hinaus in Weite" findet das christliche Treffen von Mittwoch 21. Mai bis Sonntag, 25. Mai 2008 in Osnabrueck statt.(AP Photo/Joerg Sarbach) ---A flag of the 97th German Catholics Day in Osnabrueck, northern Germany, is seen in front the church St. Johann in Kloster Oesede near Osnabrueck on Tuesday, May 20, 2008. Flag reads the slogan 'You lead us out into the wide'. Some 55,000 people are awaited daily from Wednesday, May 21 up to Sunday, May 25.(AP Photo/Joerg Sarbach)
Bendera ya Mkutano wa 97 wa Siku ya Wakatoliki unaofanywa Osnabrück,kaskazini ya Ujerumani Mei 21 - 25 2008.Picha: AP

Mpende jirani yako kama unavyojipenda - na tenda wema kwa jamii - ni nguzo isiyokutikana katika dini ya kikristo peke yake.Kwani hata dini zingine kama vile ya Kiislamu, waumini wake wanahimizwa kushughulikia wanyonge, masikini na jamii nzima.

Kwa maoni ya Askofu Franz Vorrath kutoka mji wa Ujerumani Essen,hali ya wasi wasi na hofu iliyopo kati ya Wakristo na Waislamu ni hali inayokutikana hata katika huduma za kijamii katika dini zote mbili.Anasema,kwa upande mmoja,Waislamu wanaamini kuwa taasisi za makanisa kama vile chekechea,shule na hospitali ni vyombo vinavyotumiwa kueneza Ukristo;upande mwingine,Wakristo wengi wanaamini kuwa dini ya Kiislamu haijihusishi na masuala ya kijamii.Na mkutanoni imedhihirika kuwa hoja zote mbili hazina msingi.

Askofu Franz Vorrath anaesimamia pia Halmashauri ya mkutano wa maaskofu wa Ujerumani inayohusika na midahalo kati ya dini mbali mbali,kwanza amekumbusha mzizi wa amri ya Mungu kumpenda jirani na vipi Caritas-taasisi ya kanisa ilivyoanzishwa.Akamnukuu Mathias katika Injili: "Mlichowatendea ndugu zangu mmenitendea na miye pia.Kumhudumia jirani yako ni amri ya Mungu,bila ya kujali ikiwa anaamini Mungu au la."

Taasisi ya kanisa,Caritas inayotoa misaada,ilizinduliwa wakati wa shida katika karne ya 19 nchini Ujerumani. Wakristo walihimizwa kujijumuisha na kuwasaidia masikini na wagonjwa.

Na hata katika Quran kuna hadithi nyingi zinazoshauri kumshughulikia jirani yako.Profesa Abdullah Takim wa Fani ya dini ya Kiislamu kwenye chuo kikuu cha Frankfurt alinukuu aya ya Quran inayosema,"Huwezi kuwa muumini kabla ya kwanza kumshughulikia na kumuenzi jirani yako."

Nadeem Elias wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Ujerumani anaeleza kuwa hata katika dini ya Kiislamu kuna mashirika ya kuhudumia jamii kama Caritas inavyofanya. Akayataja mashirika ya misaada ya misikiti inayokusanya fedha kuwasaidia watu wenye shida.Misikiti yote 2,000 nchini Ujerumani ina mashirika kama hayo.

Mafunzo ya Kiislamu yanashadidia anaetaka kuimarisha uhusiano katika jamii yake anaimarisha uhusiano wa jamii kwa jumla.