1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya Gaza- Umoja wa Mataifa wapitisha azimio

Eric Kalume Ponda9 Januari 2009

Watu 12 wameuawa kufuatia mashambulizi makali ya wanajeshi wa Israel katika maeneo ya Gaza licha ya baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kupitisha azimio la kusitishwa kwa vita katika eneo hilo la Mashariki ya Ka

https://p.dw.com/p/GV1c
Wanajeshi wa Isreal wakiingia maeneo ya GazaPicha: AP


Mashambulizi hayo yaliendelea usiku kucha katika pande zote mbili huku Israel ilkishambulia eneo la kati kati mwa mji wa Gaza. Shambulio hilo lilijibiwa vikali na wafuasi wa chama cha Hamas waliorusha mizinga iliyoshambulia mji wa BeerShaeva yapata umbali wa kilomita 40 kutoka mpaka wa Gaza na Israel.


Azimio hilo lilopitisha kwa kauli moja na linataka kukomeshwa mara moja mapigano hayo, ambayo hadi kufikia sasa yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 800 na wengine 3000 kujeruhiwa na pia lilitaka kuondolewa kwa wanajeshi wa Israel kutoka ardhi ya Gaza.

Hali kadhalika, baraza hilo la Usalama linataka kurejewa mara moja na bila ya kutatizwa kwa shughuli za misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.


Hata hivyo, Marekani ambayo ni mshirika mkuu wa Israel haikupiga kura wakati wa kupitishwa azimio lililoafikiwa baada ya mashauriano ya muda mrefu baina ya wajumbe kutoka mataifa ya Kiarabu na wale wa kutoka mataifa ya magharibi.


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Condollezza Rice alisema kuwa Marekani inaunga mkono kikamilifu mpango ulioanzishwa na Misri wa kuleta amani ya kudumu katika eneo hilo.

Rice alisema ...``Marekani iliona kuwa kuna umuhimu wa kusubiri matokeo ya juhudi za upatanishi ili kuweza kutathmini kinachoungwa mkono na azimio hili ndio maana tukaamua kutoliidhinisha´´.


Barala la mawaziri la Israel linatarajiwa kukutana hivi leo kujadilia azimio hilo la baraza la usalama la Umoja wa mataifa lililopishwa jana usiku. Balozi wa Israel katika baraza hilo la Usalama Gabriela Shalev alisisitiza kuwa Israel haipasi kulaumiwa kwa hali ilivyo katika eneo la Mashariki ya kati kwani inatekeleza wajibu na haki ya kuwalinda raia wake.


Gabriela Shalev alisema..`` Jamii ya kimataifa sharti itilie maanani suala la Hamas kusitisha vitindo vya kigaidi na kuwaeleza bayana kuwa kundi la kigaidi kamwe haliwezi kuwa halali katika uongozi. Kipindi cha miaka minane iliyopita kilichogubikwa na mashambulio kadhalika amani ya muda mfupi kimetufunza kwamba makubaliano yoyote yale sharti yaheshimiwe na kutimizwa kadhalika kusitishwa kwa ufyatuaji wa makombora´´.

Majeshi ya Israel yamefanya mashambulizi ya usiku kucha katika zaidi ya vituo 50 vilivyoko mji wa Gaza vinavyodaiwa kuwa maficho ya silaha na maeneo ya kuundia silaha ya wanachama wa Hamas. Watu 12 waliuawa wakati wa shambulizi hilo katika upande wa Gaza, baada ya watu 20 kuuawa katika upande wa Israel kufuatia mashambulizi ya mizinga ya roketi kutoka upande wa Hamas.


Israel inasema kuwa imewapoteza jumla aya wanajeshi wake 11 na raia watatu tangu mashambulizi hayo yaanze tarehe 27 mwezi uliopita.


Wakati huo huo hali inazidi kuwa mbaya kwa wakimbizi na raia waliokwama kwenye mashambulizi hayo baada ya mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu kusimamisha shughuli zao katika eneo hilo hapo jana.


Hatua hii ilichukuliwa kufuatia kuuawa kwa wafanyi kazi wawili wa mashirika hayo. Hata hivyo shirika la msalaba mwekundi limesema kuwa litatoa huduma chache katika eneo la kati kati mwa mji wa haza hadi pale litakapohakikishiwa usalama wake.


Mashambulizi hayo bado yanaendelea kupingwa vikali huku maandamano ya kuipinga Israel yakiandaliwa katika miji na nchi mbali mbali za Uliwengu.


Maelfu ya maafisa wa usalama wamepelekwa katika eneo la mashariki mwa mji wa Jerusalem baada ya Hamas kutangaza maandamano makubwa katika eneo hilo.